BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAISHA YA MWANASOKA HODARI, PELE NA MAISHA NJE YA SOKA YANASIKITISHA !



Na Geofrey Chambua.
Kwa watu wengi, Pele ni mchezaji bora zaidi kuwahi kushuhudiwa katika uwanja wa kandanda, na siyo bure kwamba walimpa jina la utani kama mfalme “O Rei“.

Habari isiyo njema ni kwamba gwiji huyu wa Soka kwa miongo kadhaa Duniani sasa anatembea kwa usaidizi wa kiti cha magurudumu matatu.

Pele aliiisadia Brazil kutwaa taji la soka duniani kwa mara tatu mnamo mwaka 1958, 1962 na1970.

Afya ya Pele imeendelea kudhoofika ka miaka ya karibuni na na hasa aiposhindwa kuhudhuria uzinduzi wa Michezo ya Olimpiki mnamo mwaka 2016 kutokana na kuugua.

Jina lake halisi ni Edison Arantes do Nascimento. Alicheza kama mshambuliaji wa kati. Akiwa na miaka 17 tu aliisaidia Brazili kutwaa kombe la dunia 1958 na baadaye tena 1961 na baadaye mwaka 1970.
Aliweka rekodi mwaka 1958 ya kuwa mchezaji mdogo kuliko wote duniani kucheza katika fainali ya kombe la dunia alipocheza akiwa na umri wa miaka 17. 


Alivuma sana katika miaka ya 1970 duniani kote. Alifunga mabao 1,281 katika mechi 1,363 alizocheza kwa miaka 21yakiwemo mabao 77 katika mechi 91 alizoichezea Timu ya Taifa ya Brazil kabla ya kustaafu rasmi soka la ushindani

Mpaka sasa dunia imekuwa ikiwaita wachezaji hawa wafalme kwenye soka, Pele, Diego Maradona na Lionel Messi. 


Hivi karibuni mbrazili Pele amesema yeye tu ndio mfalme na kwamba kama yeye ni mfalme basi Messi ni mtoto wa kiume wa mfalme ambaye ni Prince.
Wakati fulani Waingereza waijaribu kumfananisa Nahodha wao na Pele na Wabrazil wakajibu kwa dhihaka kwaba itawachukua karne nzima kumpata Pele mwingine ima ni wa kuchongesha ama wa kuumba (katuni) kwenye michezo ya Komputa.


Kwa watu wengi, Pele ni mchezaji bora zaidi kuwahi kushuhudiwa katika uwanja wa kandanda, na siyo bure kwamba walimpa jina la utani kama mfalme “O Rei“.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: