BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WATOTO 10 WAZALIWA KATIKA MKESHA WA MWAKA MPYA 2012 MANISPAA YA MORO.


Mkazi wa Mwembesongo Manispaa ya Morogoro, Siwema Amri (21) akiwa amekipakata kichanga chake katika wodi ya wazazi hopsitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro mara baada ya kujifungua katika mkesha wa mwaka mpya 2012 ambapo jumla ya watoto tisa walizaliwa, wanane wakiwa wa kike na mmoja wa kiume mkoani hapa.

HABARI:
JUMLA ya watoto 10 wamezaliwa katika mkesha wa mwaka mpya wa 2012 katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro huku mmoja akizaliwa katika kituo cha afya cha Mafiga mkoani hapa.

Akizungumza na gazeti hili hospitalini hapo mkoani hapa, Afisa muuguzi msaidizi daraja la pili, Zaituni Pwetete alisema jumla ya watoto tisa wamezaliwa katika hospitali ya wazazi ya mkoa huo katika mkesha wa mwaka mpya 2012.

Pwetete alisema kati ya watoto hao tisa watoto nane ni jinsia ya kike huku mmoja akiwa wa jinsia ya kiume ambapo watoto nane walizaliwa kwa njia ya kawaida huku mmoja akizaliwa kwa njia ya operesheni.

“mwaka mpya 2012 watoto waliozaliwa ni tisa tu kati yao wakiume mmoja na kike nane lakini katika hao watoto nane walizawaliwa kwa njia ya kawaida huku mmoja akizaliwa kwa njia ya operesheni na hao wote wanaendelea vizuri” alisema Pwetete.

Wakati katika kituo cha afya cha Mafisa Manispaa ya Morogoro ni mtoto mmoja aliyezaliwa katika mkesha huo wa mwaka mpya 2012 na kufanya jumla ya watoto 10 waliozaliwa katika mkesha huo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: