BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

PINDA AZINDUA MAONYESHO YA WAKULIMA KANDA YA MASHARIKI UWANJA WA MWL JULIUS NYERERE NANE NANE MOROGORO.

 WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA akiwahutubia wananchi waliojitokeza katika ufunguzi wa maonyesho ya wakulima kanda ya mashariki inayoundwa na mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani na Morogoro katika viwanja vya Mwl Julius Nyerere Nane Nane mkoani Morogoro.
Waziri  mkuu Mizengo Pinda kulia akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tanseed International, Isaka Mashauri juu ya mbegu ya zao la mpunga aina ya TXD 306 (SARO5) wenye uwezo wa mavuno tani sita kwa hektari moja wakati waziri mkuu huyu alipotembelea banda kampuni ya uzalishaji wambegu bora za mahindi katika maonyesho ya wakulima ya nane nane kanda ya mashariki uwanja wa Mwl Julius Nyerere mkoani Morogoro.
Pinda kulia akiangalia kilimo mseto cha mahindi na mbaazi wakati alipotembelea banda hilo la Tanseed Internationali kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Isaka Mashauri na katikati ni Mwenyekiti wa Taso kanda ya Mashariki, Mohamed Mzee.
 Hapa Pinda akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya mbegu bora ya Tanseed International Morogoro, Isaka Mashauri juu ya teknolojia ya mbegu ya mahindi ya chakula malisho (FOOD-FEED) katika banda hilo wa kwanza kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera.
 Waziri mkuu Mizengo Pinda na Mwenyekiti wa Taso kanda ya Mashariki, Mohamed Mzee kulia wakati msafara wa mkuu huyu ulipofika katika  banda Water for Third word (W3W)katika maonyesho hayo.
Waziri mkuu Mizengo Pinda kulia, Katibu wa Taso Raphael Jackson na mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera wakati kutembelea mabanda ya maonyesho mbalimbali katika ufunguzi huo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment