BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WATU 14 WAFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA EBOLA NCHINI KONGO DRC.

 RAIS JOSEPH KABILA.

File:Joseph kabila.jpg  



DADI ya watu waliouawa kwa homa ya ebola huko kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeongezeka na kufikia 14 huku mripuko huo ukiwa bado haujadhibitiwa.

Shirika la Afya Duniani WHO limetangaza kuwa kitovu cha mripuko wa homa hiyo ya ebola ambayo awali mwezi uliopita ilimuuwa mhanga wake wa kwanza, ni mji wenye shughuli nyingi wa Isiro katika mkoa wa Orientale, hata hivyo homa hiyo imeenea pia huko Viadana mji ulioko umbali wa kilomita 75 kutoka mjini Isiro. 

WHO pia imeomba msaada wa karibu dola milioni mbili ili kusaidia sekta dhaifu ya afya ya Kongo kukabiliana na maradhi hayo.
Maafisa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwezi uliopita walithibitisha kuwa homa ya ebola iliyoiathiri hivi sasa nchi hiyo inatofautiana na ile iliyouwa watu wasiopungua 36 katika nchi jirani ya Uganda ambayo inaaminika kuenezwa na wenyeji wanaokula nyama yenye maambukizi ya ugonjwa huo msituni.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: