Mshambuliaji
wa timu ya soka ya Mbeya City ya mkoani Mbeya John Kanda kushoto
akiwania mpira dhidi ya mlinzi wa Burkina Fc Hamis Omari wakati wa
mchezo wao wa ligi daraja la kwanza uliofanyika kwenye uwanja wa Jmahuri
mkoa wa Morogoro ambapo katika mchezo huo Mbeya City ilishinda kwa bao
1-0.
Mlinda Mlango wa Burkina FC ya mkoani Morobgoro Ramadhan Barakati kulia
akijiandaa kudaka mpira dhidi ya washambuliaji wa Mbeya City ya jijini
Mbeya wakati wa mchezo wao wa ligi daraja la kwanza uliofanyika kwenye
uwanja wa Jmahuri mkoa wa Morogoro ambapo katika mchezo huo Mbeya City
ilishinda kwa bao 1-0.
TIMU
ya ya soka ya Burkina FC imenza vibaya ligi daraja la kwanza baada ya
kukubali kipigo kutoka kwa Mbeya City ya mkoani Mbeya katika mchezo
mkali wa ufunguzi wa ligi hiyo uliofanyika kwenye uwanja wa jamhuri na
kulala kwa bao 1-0 mkoani Morogoro.
Katika
mchezo huo Burkina FC walishindwa kutengeneza mashambulizi ya kutosha
kutokana na safu yake ya kiungo kushindwa kutengeneza mipira kwa
washambuliaji wao na kuwapa mwanya Mbeya City kutawala eneo hilo.
Mbeya
City ndiyo walionekana kutwala mchezo huo kwa vipindi vyote viwili kwa
kufanya mashambulizi ya mara kwa mara katika lango la Burkina FC na
kuwapa wakati mgumu walinzi na mlinda mlango wa timu hiyo Ramadhan
Barakati aliyefanya kazi ya ziada ya kupangua michomo ya washambuliaji
wa timu pinzani.
Katika
mchezo huo Mbeya City walifanya mashambulizi ya nguvu ya hatari katika
lango la Burkina FC katika dakika ya 32, 49 na 50 kwa washambuliaji wake
kushindwa kuzifumania nyavu kabla ya kufanya shambulizi lililozaa bao
katika dakika ya lililofungwa kiurahisi na nahodha wa Mbeya City Hassan
Mwasapili baada ya kuwapiga chenga walinzi na mlinda mlango wa Burkina
FC Mohamed Barakati kufuatia pasi ya Hassan Mwasapili.
Burkina
FC walifanya shambulizi moja la nguvu ambalo lingezaa kuzaa bao katika
dakika ya 21 kwa mpira wa adhabu ndogo nje ya 18 uliopigwa kiufundi na
kiungo, Stanley Nyangile na mpira huo kuokolewa na mlinda mlango wa
Mbeya City, Aman Simba na kuwa kona ambayo haikujazaa matunda.



0 comments:
Post a Comment