BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KAPUYA ALIDAI GAZETI SH5MILIONI


 Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya.

MBUNGE wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya ametoa muda wa siku 14 kwa gazeti moja jina (linahifadhiwa) litolewalo kila wiki kumwomba radhi na kumlipa fidia ya Sh5 bilioni kama halitatekeleza.
Ametoa tamko hilo kwa maelezo kwamba gazeti hilo lilimdhalilisha kwa kumhusisha na Watanzania wanaodaiwa kuficha mabilioni ya fedha nchini Uswis.
Profesa Kapuya, alilitaka gazeti hilo kumwomba radhi na kumlipa fidia hiyo kutokana na kuandika habari iliyomtaja kuwa ni mmoja Watanzania wanaodaiwa kuficha pesa nchini Uswis, habari ambayo alisema kuwa ni ya uongo.
Kupitia kwa Wakili, Yassin Membar wa Kampuni ya Uwakili ya Membar Law Attorneys, Profesa Kapuya ameliandikia gazeti hilo barua ya kusudio la kuliburuta mahakamani iwapo halitatekeleza amri yake ndani ya muda huo.
Katika barua hiyo Profesa Kapuya ambaye amewahi kushika wadhifa wa Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, katika Serikali ya awamu ya nne, alisema habari hiyo imemsababishia madhara makubwa na imemshushia heshima.
Pia alidai kuwa maneno yaliyoandikwa kwenye habari hiyo kuhusu mteja wake ni ya uongo ambayo ililenga kumchafulia jina mteja wake, kumshushia heshima yake na kumchonganisha na wananchi na kwamba imemsababishia usumbufu mkubwa na imemletea madhara kiafya.
Kwa mujibu wa barua hiyo, habari hiyo inayolalamikiwa ni ile iliyoandikwa na gazeti hilo toleo lake Na.207 la Jumatatu, Novemba 12-18, 2012.
Habari hiyo iliyochapishwa katika ukurasa wa mbele na kuendelea katika ukurasa wa 16, 17 na 18, ilikuwa na kichwa cha habari kisemacho “Vigogo wa mabilioni ya Uswis hawa hapa.”

Katika barua hiyo, wakili huyo wa Kapuya alisema kuwa mbali na kichwa hicho cha habari pia kulikuwa na picha za vigogo hao, ikiwamo ya mteja wake, Profesa Kapuya ambayo anadai kuwa ni kama ushahidi wa habari hiyo.

Kwa mujibu wa barua hiyo, habari hiyo pia ilimnukuu Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, wakati akizungumzia sakata hilo la watuhumiwa wa mabilioni hayo ya Uswis.

“Zitto alieleza zaidi kuwa wengine ambao mali zao zinapaswa kuchunguzwa kwa kina na Serikali ni waliopata kushika wadhifa wa uwaziri wa ulinzi na ukuu wa majeshi katika kipindi hicho cha mwaka 2003 hadi 2010.”, inasomeka barua hiyo ikimrejea Kabwe.
CHANZO GAZETI LA MWANANCHI.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: