Magari yakiwa yanateketea kwa moto mkoani Mtwara.
Nyumba ikiteketea kwa moto mkoani Mtwara hii leo katika vurugu zilizozuka.
WATU watatu wamefariki dunia Mkoani Mtwara baada ya kutokea
vurugu kubwa kati ya Askari wa Jeshi la Polisi na waendesha Pikipiki
maarufu (Bodaboda).
Taarifa za tukio hilo zilizotufikia hivi Punde zinadai kwamba vurugu hizo zimesababishwa na Askari Poli
kumkamata mmoja wa dereva bodaboda hao na kuanza kumpiga kiasi cha
kupoteza fahamu.
Mbali na watu hao waliouwawa katika
vurugu hizo taarifa hiyo pia imeeleza kuwa zaidi ya nyumba na
ofisi tatu za serikali pamoja na magari matano yamechomwa moto.
Tunaendelea kuzifuatia taarifa hizo kwa kina na tutaendelea kuwajulisha hivyo endeleeni kufuatilia kwa undani wake.
Chanza Habarimpya.com
0 comments:
Post a Comment