BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KAKAKUONA ALIYEONEKANA HOSPITALI YA MKOA WA MOROGORO AHIFADHIWA MALIASILI.



Kakakuona akiwa katika mikao tofauti moja ya chumba cha wagonjwa wenye matatizo ya akili katika hospitali ya mkoa wa Morogoro muda mfupi kabla maafisa wa Maliasili mkoa kuchumchukua na kwenda kumhifadhi kiumbe huyo anayeonekana kwa nadra sana.

Kakakuona huyo ambaye alionekana majira ya saa 2 usiku jana katika maeneo ya hospitali hiyo, leo asubuhi aliwekewa nafaka, panga, maji, jembe, unga na maji ambapo kutokana na kuweka hivyo hiyo kakakuona huyu alichagua.

Mnyama huyu alifanikiwa kuchagua maji kwa kuyanywa na baadae kuyakoroga ikiwa ni chaguo lake la kwanza la utabiri ambapo ishara hiyo ikitafsiliwa kuwa mwaka ambao mvua zitakuwa nyingi sambamba na mafuliko kisha  kuendelea na chaguo la pili ambalo ni jembe akitabiri kuwa mwaka wa wakulima wavuna mazao mengi. 
                          
Katibu Tawala mkoa wa Morogoro, Eliya Ntandu (mbele) akichukua picha ya Kakakuona huyo. 

Baadhi ya manesi na wananchi katika Manispaa ya Morogoro wakimwangalia kiumbe huyo ambaye amevuta hisia ya wakazi wa mjini hapa.
Deus Mfipa akiwa amembeba kakakuona kutoka kwenye chumba hicho na kumtoa nje.
Mkazi wa Mikese wilaya ya Morogoro, Deus Mfipa akijiandaa kumbeba kiumbe huyo mara baada ya Katibu Tawala mkoa wa Morogoro, Eliya Ntandu kumshuhudia kabla ya maafisa wa maliasili kumbeba.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: