BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KIKONGWE AJINYONGA KWA UGUMU WA MAISHA MOROGORO.



 
PICHA YA MAKTABA IKIONYESHA MTU AKIWA AMEJINYONGA LAKINI PICHA HII HAIUSIANI NA TUKIO LA KUJINGOA KWA KIKONGWE MOROGORO.

WATU watano wamefariki dunia mkoani hapa katika matukio tofauti, likiwemo la mzee mmoja kufa baada ya kujinyonga na kamba kutokana na ugumu wa maisha.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Fustine Shilogile, alimtaja marehemu huyo kuwa ni Yohana Malunda (73), mkazi wa Mfulu, wilayani Kilosa.

Alisema tukio hilo lilitokea Januari 22 mwaka huu, saa11 jioni katika Kijiji cha Mafulu, Kata ya Kitete wilayani Kilosa, ambapo mtu huyo alijinyonga kwa kutumia kamba iliyosokotwa kwa mlala na kuifunga katika dari la nyumba yake.

Alisema tukio jingine ni lile lilitokea Januari 21 mwaka huu katika Kituo cha Afya Dutumi, Wilaya ya Morogoro Vijijini, ambapo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Juma Kilatwa (25) alifariki dunia baada ya kung’atwa na mamba.

Alisema mtu huyo aling’atwa na mamba sehemu za kichwani, mgongoni na kifuani, akiwa katika mto Ngeta, uliopo katika Kijiji cha Dakawa.

“Hali hiyo ilisababisha kuvuja damu nyingi na kusababisha kifo chake, akiwa kituo cha afya wakati akipatiwa matibabu,” alisema Kamanda Shilogile.

Kamanda Shilogile alisema tukio la tatu lilitokea Januari 21, eneo la kivuko cha reli Modeko, Manispaa ya Morogoro ambapo askari mwenye namba E 9036 SGT Isaya Daniel Lukindo (42) aligonga kiberenge na kufariki dunia.

Alisema askari huyo alikuwa akiendesha pikipiki yenye namba za usajili T763 aina ya Elerical Stater CDI, ambapo aligonga kiberenge namba HDT.2 na hivyo kusababisha kifo chake.

Katika tukio jingine, kamanda huyo alisema lilimhusisha mwanamume mmoja aliyefahamika kwa jina la Juma Kidevu, anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 35 hadi 45.

Alisema mtu huyo alikutwa amekufa katika nyumba ambayo bado haijaisha maarufu kama pagala, huku mwili wake ukiwa hauna jeraha lolote na kwamba chanzo cha kifo hicho bado hakijajulikana.

Kamanda Shilogile alisema tukio la tano lilitokea Januari 22, saa 1 usiku eneo la stendi ya mbuzi Ruaha, wilayani Kilosa, ambapo mwendesha pikipiki alimgonga mtembea kwa miguu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: