WAZIRI Mkuu aliyejiuzuru Edward Lowassa ametetea waarifu nchini
na kudai kuwa hakuna haja ya kuwepo kwa adhabu ya kifo Tanzania, badala yake
iwepo ibara katika katiba mpya itakayotamka wazi kwamba hakutakuwa na adhabu ya
kifo hapa nchini kwa kosa la kukusudia au uhaini.
Akizungumza mbele ya tume ya kukusanya maoni ya Katiba mpya jijini
Dar es Salaam muda mfupi uliopita Lowassa alisema kwamba, katiba ya sasa
haisemi wazi kuhusu adhabu ya kifo na kwamba inazungumzia tu haki ya uhai
katika ibara ya 14 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
"Katiba ya
sasa inatamka kiujumla tu kuwa kila mtu ana haki ya kuishi na uhai wake
kulindwa lakini, haki hiyo haitekelezwi kufuatia kifungu namba 196 cha sheria
ya kanuni za adhabu ya sura ya 16, (penal code, cap 16) kinachotamka kuwa
adhabu ya kifo(death penalty or capital punishment)"alisema Lowassa.
Kuhusu kosa la
mauaji ya kukusudia Lowassa alisema kwamba, adhabu hiyo pia utolewa kwa kosa la
uhaini. hivyo alipendekeza kwamba kuwe na ibara katika katiba mpya itakayotamka
wazi kwamba hakuna adhabu ya kifo Tanania.
CHANZO http://www.habarimpya.com
0 comments:
Post a Comment