BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

LOWASSA MGENI RASMI UZINDUZI WA MFUKO WA JAMII, TOVUTI YA MORO PRESS CLUB.




Mwenyekiti wa muda wa Morogoro Press Club Boninveture Mtalimbo kulia akionekana katika picha tatu tofauti akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari juu ya shughuli za uzindizi wa mfuko  wa jamii, uzinduzi wa Tovuti ya chama na bonanza la kukaribisha mwaka mpya 2013 na kuaga mwaka 2012 zinazotarajia kufanyika januari 19 mwaka huu mkoani hapa. kushoto ni Mratibu wa miradi katika chama hicho Thadei Hafigwa.
 Mwandishi na mtangazaji wa IPP MEDIA mkoa wa Morogoro Idda Moshi kusho akichangia jambo katika mkutano huo na kulia ni Mratibu wa miradi katika chama hicho Thadei Hafigwa.
 Mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi mkoa wa Morogoro Hamida Shariff kushoto akieleza jambi katika mkutano huo, kulia ni Lilian Chuwa wa gazeti la Majira Morogoro.
Mwandishi Lilian Chuwa wa gazeti la Majira Morogoro akifuatilia jambo na Lilian Lucas wa Mwananchi wakati wa mkutano huo ambao ulihudhuriwa na waandishi mbalimbali.
 Mwandishi wa shirika la utangazaji la TBCI mkoa wa Morogoro Monica Lyampawe akihoji jambo huku Mwandishi wa IPP MEDIA Morogoro, Safia Maftaha akifuatilia matukio mbalimbali.
Mwandishi wa IPP MEDIA Fitina Haule kushoto akichukuliwa picha na Idda Mushi kwa ajili ya kituo cha luninga cha ITV mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo.

 Na Thadei Hafigwa.
WAZIRI Mkuu Mstaafu Edward Lowasa anatarajiwa kuongoza shughuli za uzindizi wa mfuko  wa jamii pamoja na Tovuti ya chama cha waandishi wa habari mkoa wa Morogoro (MOROPC) wakati wa sherehe ya kuuaga mwaka 2012 na kuukaribisha 2013.

Hayo yalibainishwa na Mwenyekiti wa Muda wa Moropc Boniventure Mtalimbo wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye ofisi za chama hicho, nakwamba uzinduzi huo utafanyika Januari 19 mwaka huu katika hoteli ya kitalii ya   Nashera mjini Morogoro.

Alisema  lengo la kuanzishwa kwa mfuko wa jamii ni kuwawezesha waandishi wahabari, kwenda vijijini kwaajili ya kuandika habari kutokana na maeneo hayo kushindwa kufikika kwa urahisi kutokana na ukosefu wafedha.

Mtalimbo alisema mbali na waandishi kwenda vijijini pia utakuwa ukisaidia kwa mambo mbalimbali ikiwemo kwenye maafa, kama vile vifo, magonjwa pamoja na kuwawezesha kujiendeleza kielimu.

Akizungumzi uzinduzi wa tovuti (Website) alisema waandishi wa habari mkoani Morogoro watakuwa wakiandika makala mbalimbali zikiwemo za kuelimisha jamii,na kuandaa vipindi vya televisheni na redio na kuingiza kwenye tovuti hiyo.

 Aidha Mwenyekiti huyo aliwaomba wadau mbalimbali ndani nanje ya mkoa wa Morogoro, kujitokeza kuchangiakwa hali na mali mfuko huo ili kuwawezesha waandishi hao kufanya kazi kwa ufanisi zaidi pamoja na kuibua mambo mbalimbali yaliyojificha hususani vijijini.

Aliwataja wadhamini waliojitokeza hadi sasa kuwa ni Hoteli ya Nashera, Banki ya CRDB, Mamlaka ya mapato Tanzania TRA,Kampuni ya Umeme ya Mac Dolnad Live line,Kampuni ya Abood, Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini  Azizi Abood, Mamlaka ya Maji safi na Taka mkoa wa Morogoro MORUWASA.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: