WAZIRI MKUU PINDA.
Taarifa za awali zimeeleza kuwa mahabusu hao wamefikia hatua hiyo kutokana na kucheleweshwa kwa kesi zao kunakofanywa na watendaji wa Mahakama pamoja na maafisa wa magereza.
Mahabusi hao wameeleza kuwa ni vema wakafikwa na umauti kwani haki yao imekamatwa na watu wachache kwani wengine wamekaa katika gereza hilo kwa muda wa miaka mitatu wakiwa hawajui nini hatma yao.
Kufuatia tetéis hizo msemaji wa jeshi la Magereza nchini Omary Mtiga amethibitisha kutokea kwa sakata hilo na kueleza kuwa juhudi za kuwasikiliza mahabusu hao zinafanywa kwa lengo la kurejesha amani.
Aidha wadau wa mbalimbali waliohojiwa na tovuti hii wameelezea hisia zao tofauti kuwa mahabusu hao wanahaki ya kufanya hivyo kwani siku hizi mahakama zimekuwa kichwa cha mwenda wazimu.
"Haiwezekani mtu aingie mahabusu miaka mitatu alafu hafahamu hatma ya suala lake, huo upelelezi ni wa aina gani?, alihoji mkazi mmoja wa Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Endelea kuwa nasi kwa habari zaidi.
CHANZO http://www.habarimpya.com
0 comments:
Post a Comment