Mkuu wa
Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja (katikati)
akikagua gwaride la heshima la wahitimu wa mafunzo ya awali ya udereva
wa magari kozi namba 18 na udereva wa matreka kozi namba 7 katika Chuo
cha Udereva na Ufundi cha jeshi hilo (KPF) kilichopo Kingolwira nje
kidogo ya Mji wa Morogoro.
Mkuu wa
Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja akimpongeza
Beatrice Dugange baada ya kumpa cheti na leseni ya udereva baada ya
kumaliza mafunzo ya udereva chuoni hapo. Jumla ya wanafunzi 66
walipatiwa vyeti na leseni kwa kuhitimu mafunzo hayo.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja akitoa hotuba yake na baadaye kufunga mafunzo hayo ya awali.
Wanafunzi
wa Shule ya Msingi Mkono wa Mara iliyopo chuoni hapo wakitumbuiza
katika sherehe hiyo kwa kutoa michezo mbalimbali mbele ya mgeni rasmi,
Kamishna Jenerali John Minja.
Baadhi
ya wahitimu wakimsikiliza kwa makini, Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini,
Kamishna Jenerali John Minja wakati akitoa hotuba yake na baadaye
kuyafunga mafunzo ya udereva wa magari kozi namba 18 na udereva wa
matreka kozi namba 7.
PICHA ZOTE NA
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
0 comments:
Post a Comment