Kwa ufupi:
“Nimepigiwa simu nyingi usiku wa kuamkia leo,
tukio hili la kukamatwa kwa wanajeshi, limewakatisha tamaa kabisa wananchi,
wanalia wanataka mimi na kamati yangu tuingilie kati,” alisema Lembeli.
Picha ya maktaba ya membo ya tembo.
Picha ya tembo.
GARI aina ya Toyota VX linaloelezwa kuwa mali
ya Serikali limekamatwa na polisi likiwa limebeba pembe za ndovu.
Habari zilizolifikia gazeti hili jana zilieleza
kuwa gari hilo lilikamatwa juzi saa 3:00 usiku katika Kijiji cha Kigongoni
katika Mji wa Mto wa Mbu, wilayani Manyara baada ya gari hilo kupinduka.
Vyanzo vya uhakika kutoka ndani ya Jeshi na
Polisi zimeeleza kuwa askari wa jeshi hilo aliyekuwa akiendesha gari hilo
anashikiliwa na polisi.
Uchunguzi umebainisha kuwa ndani ya gari hilo kulikuwa na meno ya tembo na watu
wengine watatu ambao walikimbilia porini na baadhi ya nyara hizo.
Habari hizo zimedai bado kuna utata kuhusu
gari lililokuwa likitumiwa na maofisa hao kwa kuwa kibao cha namba za gari hilo
kinasomeka kwa namba za kiraia lakini vioo vimechorwa namba za Serikali, huku
Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa akisema pia kulikuwa na namba za JWTZ.
Kulingana na taarifa kutoka ndani ya Jeshi la
Polisi, kukamatwa kwa gari hilo kulitokana na Askari wa Shirika la Hifadhi za
Taifa Tanzania (Tanapa), Hifadhi ya Ziwa Manyara kudokezwa na raia wema.
Inaelezwa kuwa baada ya askari hao kudokezwa,
walianza kufuatilia nyendo za maofisa hao ndani ya hifadhi na walipogundua
wanafuatiliwa, gari hilo liliongeza mwendo kuelekea Mji wa Mto wa Mbu.
Hata hivyo, kutokana na mwendokasi wa gari hilo na kutokuwa wazoefu
kulinganisha na Askari wa Tanapa, gari la maofisa hao lilipinduka lilipofika
Kijiji cha Kigongoni nje kidogo ya Mto wa Mbu.
“Baada ya kupekuliwa lilikutwa na pembe mbili
za ndovu na uchunguzi wa awali umethibitisha maofisa waliokimbia walifanikiwa
kutoroka na pembe nyingine tatu,” kilidokeza chanzo hicho.
Kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kulitokana na wananchi kumtilia shaka yeye na
wenzake gari lao lilipopata ajali kwa kitendo cha watu wawili waliokuwepo
kwenye gari hilo kuonekana wakihamisha mizigo na kukimbilia porini.
“Matairi mawili ya gari yalipasuka lakini
ajabu ni kwamba wananchi walipojitokeza kusaidia majeruhi, wawili kati yao
walinyanyua mizigo isiyojulikana na kukimbilia porini huku wakimwacha mwenzao
aliyevaa sare za jeshi akisubiri garini,” alisema mtoa taarifa wetu.
Kwa mujibu wa mashuhuda, wakati wa ajali
hiyo, mtuhumiwa alikuwa amevaa jaketi la JWTZ pamoja na suruali ya jinsi akiwa
na bunduki aina ya Rifle.
Katika msako uliofanywa na polisi kwa kushirikiana na wananchi, pembe mbili
zaidi za ndovu zilikutwa zikiwa zimefichwa karibu na eneo la ajali.
Mkurugenzi mkuu wa Tanapa, Allan Kijazi
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lakini akasema hana taarifa kamili kwani
yuko Tanga na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira.
“Ni kweli nimearifiwa juujuu tu, nasubiri
taarifa kamili lakini nimeambiwa tu hilo gari lilipinduka wakati wakifukuzana
na askari wetu, lakini mnaweza mkapata taarifa zaidi polisi,” alisema Kijazi.
Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe
alisema hajapata taarifa hiyo, hivyo asingeweza kutolea maoni kwa namna yeyote.
Picha ya maktaba ya membo ya tembo. 
GARI aina ya Toyota VX linaloelezwa kuwa mali ya Serikali limekamatwa na polisi likiwa limebeba pembe za ndovu.
Habari zilizolifikia gazeti hili jana zilieleza kuwa gari hilo lilikamatwa juzi saa 3:00 usiku katika Kijiji cha Kigongoni katika Mji wa Mto wa Mbu, wilayani Manyara baada ya gari hilo kupinduka.
Vyanzo vya uhakika kutoka ndani ya Jeshi na Polisi zimeeleza kuwa askari wa jeshi hilo aliyekuwa akiendesha gari hilo anashikiliwa na polisi.
Uchunguzi umebainisha kuwa ndani ya gari hilo kulikuwa na meno ya tembo na watu wengine watatu ambao walikimbilia porini na baadhi ya nyara hizo.
Habari hizo zimedai bado kuna utata kuhusu gari lililokuwa likitumiwa na maofisa hao kwa kuwa kibao cha namba za gari hilo kinasomeka kwa namba za kiraia lakini vioo vimechorwa namba za Serikali, huku Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa akisema pia kulikuwa na namba za JWTZ.
Kulingana na taarifa kutoka ndani ya Jeshi la Polisi, kukamatwa kwa gari hilo kulitokana na Askari wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa), Hifadhi ya Ziwa Manyara kudokezwa na raia wema.
Inaelezwa kuwa baada ya askari hao kudokezwa, walianza kufuatilia nyendo za maofisa hao ndani ya hifadhi na walipogundua wanafuatiliwa, gari hilo liliongeza mwendo kuelekea Mji wa Mto wa Mbu.
Hata hivyo, kutokana na mwendokasi wa gari hilo na kutokuwa wazoefu kulinganisha na Askari wa Tanapa, gari la maofisa hao lilipinduka lilipofika Kijiji cha Kigongoni nje kidogo ya Mto wa Mbu.
“Baada ya kupekuliwa lilikutwa na pembe mbili za ndovu na uchunguzi wa awali umethibitisha maofisa waliokimbia walifanikiwa kutoroka na pembe nyingine tatu,” kilidokeza chanzo hicho.
Kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kulitokana na wananchi kumtilia shaka yeye na wenzake gari lao lilipopata ajali kwa kitendo cha watu wawili waliokuwepo kwenye gari hilo kuonekana wakihamisha mizigo na kukimbilia porini.
“Matairi mawili ya gari yalipasuka lakini ajabu ni kwamba wananchi walipojitokeza kusaidia majeruhi, wawili kati yao walinyanyua mizigo isiyojulikana na kukimbilia porini huku wakimwacha mwenzao aliyevaa sare za jeshi akisubiri garini,” alisema mtoa taarifa wetu.
Kwa mujibu wa mashuhuda, wakati wa ajali hiyo, mtuhumiwa alikuwa amevaa jaketi la JWTZ pamoja na suruali ya jinsi akiwa na bunduki aina ya Rifle.
Katika msako uliofanywa na polisi kwa kushirikiana na wananchi, pembe mbili zaidi za ndovu zilikutwa zikiwa zimefichwa karibu na eneo la ajali.
Mkurugenzi mkuu wa Tanapa, Allan Kijazi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lakini akasema hana taarifa kamili kwani yuko Tanga na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira.
“Ni kweli nimearifiwa juujuu tu, nasubiri taarifa kamili lakini nimeambiwa tu hilo gari lilipinduka wakati wakifukuzana na askari wetu, lakini mnaweza mkapata taarifa zaidi polisi,” alisema Kijazi.
Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe
alisema hajapata taarifa hiyo, hivyo asingeweza kutolea maoni kwa namna yeyote.

0 comments:
Post a Comment