Mbeba mizigo katika soko kuu la mkoa wa Morogoro akiwa amebeba gunia la
vitunguu wakati akifanya kazi ya kusomba kutoka kwenye gari kwenye baada
ya kupata kazi hiyo na mwaajili wake ambapo gunia moja hutozwa kiasi
cha sh1,000 mkoani hapa.
Wanafunzi wa shule ya awali ya Wesley Primary School, Salma
Mtanda kulia na Shariffa Mkundanga wote miaka (6) wakiwa na maboksi ya
zawadi mara baada ya kuzawadi na familia zao wakati wa mahafali ya
kuhitimu elimu hiyo ili kuweza kuanza elimu ya msingi iliyofanyika
shuleni kwao Nyandila Kihonda Morogoro.
Wanafunzi wa shule ya msingi Ipera Asilia wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro wakiwa wamebeba matofali ya kuchoma wakati wakifanya kazi ya kusomba kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa nyumba ya mwalimu ikishirikiana na nguvu za wananchi na serikali ikiwa njia mojawapo ya kivutio kwa walimu mkoani hapa.
Mkuu wa wilaya ya Morogoro Said Amanzi mbele akiangalia gari lake likipita pembeni mwa mtaro baada ya kutumia kutokana na utelezi wakati mkuu huyo akiwa katika ziara ya utambuzi wa idadi ya mifugo tarafa ya Ngerengere na timu ya kamati ya ulinzi na usalama mkoani hapa.
Mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi Morogoro, Hamida Shariff akizungumza jambo na mwanafunzi wa darasa la nne shule ya msingi Bungo Morogoro, Mikidadi Mtanda kuhusu namna ya kuzingatia masomo na kuacha michezo isiyo na faina wakati mwanafunzi huyo alipomtembelea shangazi yake katika ofisi za gazeti hilo mkoani hapa.
Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la wizara ya kazi na vijana makao makuu, Amosi Nyandwi akimnong'oneza jambo mjumbe wa chama hicho, Msifu Chenjela kulia wakati wa semina ya vingozi wa matawi ya Tughe mkoa wa Dar es Salaam iliyofanyika ukumbi Edema mkoani Morogoro.
Raia wa kigeni kulia wakisikiliza jambo wakati mwenyeji wao (mwenye sharti nyeupe) akiongea na wafanyakazi wa kampuni ya maegesho ya Makumila kushoto baada ya kulifunga gari la raia hao kwa madai ya kuegesha eneo lisiloruhusiwa mtaa wa Lumumba eneo la stendi kuu ya daladala yanaendayo nje ya Manispaa ambapo wamekuwa wakitoza faini kiasi cha sh50,000 mkoani Morogoro .
Raia wa kigeni akizungumza na vijana wanaoishi katika mazingira magumu wakati vijana hao wakimshawishi ili waweze kumuoshea gari yake ili kupata pesa za kujimu na maisha ambapo kazi hiyo huifanya mtaa wa Makongoro eneo la CCM wilaya Manispaa ya Morogoro.
0 comments:
Post a Comment