AMTUMA WASIRA KUSULUHISHA WAISLAM, WAKRISTO.
MZOZO WA KIIMANI WAZUSHA MTAKARUKU SHULENI.
RAIS KIKWETE
MGOGORO wa udini unaoendelea kulitikisa taifa, umeonekana wazi kumshtua Rais Jakaya Kikwete, ambaye amelazimika kumtuma Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wasira, kwenda mkoani Mwanza kukutana na viongozi wa madhehebu yote ya dini.
Hatua ya Rais Kikwete kumtuma Waziri Wasira, imekuja siku chache baada ya kuibuka mvutano mkali kati ya Waislamu na Wakristo kuhusu kuchinja wanyama.
Kutokana na hali hiyo, Rais Kikwete amemtuma Waziri Wasira ambaye ameondoka leo asubuhi kwenda mkoani Mwanza kukutana na viongozi wa madhehebu yote.
Habari za kuaminika zilizopatikana kutoka Ikulu mjini Dar es Salaam, zinasema Waziri Wasira anatarajia kuwasili kwa ndege leo na moja kwa moja kukutana na viongozi hao, ili kuondoa tofauti zilizopo.
“Waziri Wasira anaondoka kwenda Mwanza kesho (leo), kwa ajili ya kukutana na viongozi wa madhehebu yote ya kidini mkoani Mwanza, tunatarajia atatumia uwezo wake wote ili kuona wananchi wanaishi kwa amani.
“Taarifa tulizo nazo ni kwamba, kikao hicho kimeandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo… kama utakumbuka hivi sasa kuna mvutano mkubwa kati ya Waislamu na Wakristo,” kilisema chanzo chetu.
Hatua ya Waziri Wasira kwenda huko, inatokana na Mkuu wa Mkoa huo, Mhandisi Ndikilo, kutoa kauli ya utata mwishoni mwa mwezi uliopita, ambapo aliwataka Waislamu ndio waendelee kuchinja na Wakristo wasifanye hivyo.
“Unajua mwishoni mwa mwezi uliopita, RC Ndikilo alikwenda katika eneo la Nyehunge na kukuta kuna bucha za Waislamu na Wakristo, lakini kubwa zaidi ni pale alipokuta mchungaji mmoja amechinja ng’ombe, kutokana na ugeni wake aliokuwa nao, jambo hilo lilizua mambo mengi.
“Baada ya kuona hivyo, Ndikilo alitamka bila wasiwasi kwamba Waislamu ndio wenye haki ya kuchinja, kauli hii ilisababisha azomewe na watu waliokuwa wamekusanyika pale na kuamua kuondoka,” kilisema chanzo chetu.
MTANZANIA ilipomtafuta Waziri Wasira ili kupata ukweli wa safari yake, alikiri na kusema lengo ni kutaka kuona Watanzania wanaishi kama ndugu.
“Naondoka kwenda Mwanza kesho (leo), kwa ajili ya kukutana na viongozi wote wa dini ili kuzungumza nao masuala mbalimbali, tunataka kuona Watanzania tunaishi kama ndugu, maana ndivyo tulivyolelewa na kukua katika mazingira haya,” alisema Waziri Wasira.
Alipoulizwa ni sababu gani kubwa iliyomsukuma, Waziri Wasira hakuwa tayari kusema zaidi ya kudai “naomba utume waandishi wako najua pale Mwanza wapo, waje wasikilize nini nasema na kisha wawajulishe Watanzania,” alisema.
Habari zaidi kutoka Mwanza, zinasema baada ya mazungumzo hayo, Waziri Wasira anatarajia kuelekea mkoani Geita, ambako nako inaelezwa hali hiyo, imeanza kujitokeza.
Mwishoni mwa mwaka jana, Padri wa Kanisa Katoliki Mpendae, visiwani Zanzibar, Ambrose Mkenda, alijeruhiwa kwa risasi na watu wasiojulikana nje ya nyumba yake wakati akitoka kanisani.
Padri huyo, alipigwa risasi akiwa ndani ya gari lake na kujeruhiwa katika sehemu ya kichwa.
Alitibiwa katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Katika tukio jingine, Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhil Soraga, alimwagiwa tindikali na watu wasiojulikana.
Kufuatia matukio hayo, viongozi mbalimbali wa Serikali walisema Serikali itawasaka kwa udi na uvumba wahusika ili wafikishwe mbele ya vyombo vya dola kujibu tuhuma zinazowakabili.
DODOMA.
Katika hali ya kushangaza, mkoani Dodoma, juzi waumini wa dini ya Kiislamu
wenye itikadi kali walivamia Shule ya Msingi Kigwe, iliyopo wilayani Bahi na
kutoboa masufuria yanayotumika kuwapikia uji wanafunzi.
Waumini hao, waliokuwa na silaha za jadi, walifikia hatua hiyo, wakidai masufuria hayo yalitumika kuchemshia maji ya kunyonyolea nguruwe.
Kabla ya kuanza kushambulia masufuria hayo, walidai Mkuu wa Shule hiyo, Mathias Mbowe, huwa anatumia moja ya masufuria kuchemshia maji ya kunyonyolea nguruwe kisha kwenda kuuza nyama mnadani.
Akizungumzia tukio hilo, Shekhe wa Wilaya ya Bahi, Hassan Khamisi, alisema waumini hao waliharibu masufuria ya shule, baada kupata taarifa kuwa moja ya masufuria hutumika kuchemsha maji ya nguruwe.
“Hali hii iliwafanya waumini wa eneo hilo ambao watoto wao wanasoma katika Shule ya Msingi Kigwe na kupatiwa uji wakiwa shuleni kupatwa na hasira kwa kuwa watoto wao wanalishwa haramu,” alisema Shekhe Khamis.
Ofisa Elimu wa Wilaya hiyo, Mary Methew, alilaani kitendo hicho akisema hakikuwa cha kiungwana kwa kuwa waumini hao walijichukulia sheria mikononi.
“Siyo kweli kwamba masufuria hayo yanatumika kwa jili ya kuchemshia maji kama walivyodai waumini hawa… kitendo cha kutoboa masufuria kitasababisha wanafunzi wa shule hiyo kukosa huduma ya kunywa uji shuleni,” alisema.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime, alikiri kutokea kwa tukio hilo.
Alisema baada ya kutokea kwa vurugu hizo, polisi walikwenda eneo la tukio, lakini walikuta waumini hao wakiwa wameshatawanyika.

Alisema polisi, wanaendelea kufanya upelelezi kuhusiana na tukio hilo.
CHANZO http://www.mtanzania.co.tz
0 comments:
Post a Comment