SERIKALI ya Uingereza inatarajiwa kujadili mpango wa kutoa
msaada zaidi kwa wanajeshi wa Ufaransa wanaopambana na waasi nchini Mali.
Waziri mkuu David Cameron, amesema kuwa huenda msaada za usafiri na kijasusi ukatolewa kwa wanajeshi hao. Ndege mbili za kijeshi tayari zimetolewa kwa jeshi la Ufaransa.
Waziri wa
ulinzi anasema kuwa hakuna mipango ya kufanya mashambuli ya ardhini kwa sasa.
Kuhusu
vifo vya raia wa Uingereza katika mashambulizi kwenye kiwanda cha gesi nchini
Algeria yaliyofanywa na wapiganaji wa kiisilamu, bwana Cameron alisema kuwa
eneo la Kaskazini mwa Afrika linageuka kuwa ngome ya wapiganaji wa kiisilamu.
Wanajeshi wa Mali wampokea msaada kutoka kwa Ufaransa na sasa Uingereza inataka pia kuwasaidia.
Wasiwasi
kuhusu athari za kundi la kigaidi la al-Qaeda katika ukanda huo, zinaonekana
kudhibitiwa kufuatia mpango wa kuwapeleka wanajeshi wa Ufaransa kupambana na
wapiganai wenye uhusiano na Al Qaeeda nchini Mali na Algeria ambako waliwateka
nyara wafanyakazi wa kigeni.
Wanamgambo
waliowashambulia wafanyakazi wa kigeni nchini Algeria, ambapo takriban mateka
48 waliuawa wametoa wito kwa Ufaransa kusitisha harakati zao nchini Mali.
''magaidi kuhangaishwa''
Waiziri
mkuu alisema kuwa Uingereza pamoja na washirika wake wako katika mapambano
dhidi ya kasumba ambayo inatia doa kubwa dini ya kiisilamu na ambayo inaamini
kuwa mauaji na ugaidi yanakubalika na tena ni sharti yafanyike.
Jibu la
jamii ya kimataifa kwa tisho hili liitakuwa swala muhimu katika ajenda ya
mkutano wa nchi nane zilizostawi duniani G8.
"lazima
tupambane na hao magaidi kwa kutumia mbinu zote za kuweka usalama, Lazima
tuwakomeshe, kijeshi.
Ni lazima tuzungumzie hii kasumba yao, sharti tufunge hii
nafasi wanayoitumia, kuendesha harakati,zao'' alisema waziri mkuu.
0 comments:
Post a Comment