BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UZINDUZI WA SHEREHE ZA MIAKA 36 YA KUZALIWA CCM, VIWANJA AFISI KUU YA CCM KISIWANDUI


 Makamu wa Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akivalishwa skafu na  Kijana Chipukizi,Pili  Hassan Suluhu, wakati alipowasili katika viwanja vya Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo asubuhi,kwa ajili ya Uzinduzi wa Sherehe za Madhimisho ya miaka 36 ya kuzaliwa kwa CCM.
 Makamu wa Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, na Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Iddi,mara alipowasili katika  viwanja vya Ofisi ya CCM Kisiwandui  Mjini Zanzibar, kuzindua sherehe za Maadhimisho ya miaka 36 ya Kuzaliwa kwa CCM,(kulia) Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Borafya Silima.
 Makamu wa Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi,waliohudhuria katika Uzinduzi wa Sherehe za Madhimisho ya miaka 36 ya kuzaliwa kwa CCM,zilizofanyika leo katika  viwanja vya Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
Makamu wa Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiongozana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai,wakielekea katika jengo la  Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja,kwa ajili ya kuweka saini kitabu cha wageni,wakati wa Uzinduzi wa Sherehe za Madhimisho ya miaka 36 ya kuzaliwa kwa CCM.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: