BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAZIRI MKUU PINDA AMJULIA HALI DCI MANUMBA, YAELEZWA HALI YAKE BADO NI TETE.

Kwa ufupi:
“Unajua bwana mkubwa alikutwa na malaria 500, ambao walisambaa mwili mzima na kuvuruga pia sehemu ya figo. Kwa sasa madaktari wanaendelea kumpatia uangalizi wa karibu ili kuhakikisha afya yake inaimarika,”. 
DCI MANUMBA
WAZIRI MKUU PINDA.

WAKATI hali ya afya ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba ikiendelea kuwa tete, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ameungana na viongozi wengine wa kitaifa kumtembelea na kupata maelezo juu ya maendeleo ya  afya yake.

Pinda alifika hospitalini hapo jana saa 6:15 mchana na kupokelewa na mmoja wa wanafamilia  kisha aliongozwa moja kwa moja hadi chumba cha Wagonjwa  Wanaohitaji Uangalizi Maalumu (ICU), alikolazwa Manumba.

Waziri mkuu alitumia dakika 15  kisha alitoka kwenye chumba hicho na kuelekea upande mwingine, ambako ilielezwa alikwenda kutia saini kitabu cha wageni na baadaye aliondoka.

Wakati anaondoka, Pinda aliwafariji ndugu na jamaa waliokuwapo eneo hilo.

Viongozi wengine ambao tayari wamefika hospitalini hapo ni   Rais Jakaya Kikwete na mke wake, Salma Kikwete.


Wengine ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi, Naibu wake, Pereira Silima, Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, Mkuu wa  Polisi, Said Mwema  na maofisa wengine wa vyeo vya juu wa jeshi hilo.

Akizungumzia maendeleo ya afya ya Manumba, mmoja wa wanafamilia, Majaliwa Mbasa alisema anaendelea kuwa chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari na wauguzi na kwamba, hali yake bado ni mbaya.

“Unajua bwana mkubwa alikutwa na malaria 500, ambao walisambaa mwili mzima na kuvuruga pia sehemu ya figo. 

Kwa sasa madaktari wanaendelea kumpatia uangalizi wa karibu ili kuhakikisha afya yake inaimarika,” alisema Mbasa.

Aliwataka wananchi kuendelea kumwombea hasa wakati huu ambao afya yake imeendelea kuwa tete.

Awali, ilielezwa kuwa kulikuwa kukiandaliwa utaratibu wa kumsafirisha nje ya nchi kwa   matibabu zaidi, lakini Mbasa alisema hilo kwa sasa haliwezekani.

“Kumpeleka nje kwa sasa katika mazingira aliyonayo haiwezekani. 

Unajua amekutwa na malaria 500, hata wewe unakumbuka kuwa Zitto Kabwe alikuwa na malaria 200, alilazwa hapahapa hadi pale afya yake ilipoanza kuimarika ndipo aliposafirishwa nje,” alisema na kuongeza.

“Hawa madaktari wataendelea kumhudumia na kama atastabilize (imarika), basi kuna uwezekano wa kupelekwa nje,”  alisema Mbasa.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: