JAHAZI la Simba limeendelea kuzama baada ya kukubali
kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Mtibwa Sugar katika mechi ya Ligi Kuu
Tanzania Bara iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji
wa Simba SC, Felix Sunzu akipiga krosi pembeni yake beki wa Mtibwa
Sugar ya Morogoro, Issa rashid katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara, jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mtibwa
ilishinda 1-0.
SIMBA NA MTIBWA SUGAR KATIKA PICHA TAIFA LEO, MNYAMA ALISHIKWA PABAYA
|
Mshambuliaji
wa Simba SC, Felix Sunzu akipiga krosi pembeni yake beki wa Mtibwa
Sugar ya Morogoro, Issa rashid katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara, jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mtibwa
ilishinda 1-0. |
|
Kocha wa Mtibwa Mecky Mexime (kulia) akitoa maelekezo kwa wachezaji wake. |
|
Kulia ni Chanongo akigombea mpira na Issa Rashid kushoto na aliyeipa mgongo kamera ni Shaaban Nditi akiwa tayari kutoa msaada |
|
Kikosi cha Simba |
|
Kikosi cha Mtibwa |
|
Salvatory Ntebe akimdhibiti Sunzu |
|
Kocha wa Simba, Mfaransa Patrick Liewig akitoa maelekezo kwa kipa na Nahodha wa timu yake, Juma Kaseja |
|
Amir Maftah akimtoka mchezaji wa Mtibwa, Jamal Mnyate |
|
Kisiga akimiliki mpira mbele ya Kapombe.
Picha kwa hisani ya http://bongostaz.blogspot.com |
JAHAZI la Simba limeendelea kuzama baada ya kukubali kipigo cha
bao 1-0 kutoka kwa Mtibwa Sugar katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara
iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Beki Salvatory Ntebe aliifungia Mtibwa Sugar bao
pekee katika dakika ya 18 akiunganisha vizuri pasi nzuri ya Vicent
Barnabas katika mchezo huo ambao Simba walimaliza wakiwa 10 baada ya
beki Juma Nyoso kupewa kadi nyekundu katika dakika ya 86.
Kwa matokeo hayo Simba imebaki ikiwa nafasi ya
tatu na pointi zake 31, huku Yanga wakiendelea kuongoza wakiwa na pointi
39, wakifuatiwa na Azam (36) katika mbio hizo za kusaka ubingwa.
Kocha wa Simba, Patrick Liewig alisema nafasi ya timu yake kutwaa ubingwa ni ndogo kwa sasa kutokana na matokeo hayo.
“Uchovu wa safari ndefu iliyoifanya timu yake hivi
karibuni mikoani na kucheza mechi za mfululizo ni sababu ya kupoteza
mchezo wa leo,” alijitetea kocha huyo.
Naye Mecky Mexime aliwasifu wachezaji wake kwa kucheza vizuri na kufanikiwa kupata ushindi huo mzuri dhidi ya Simba.
Katika mechi hiyo dakika ya pili, beki Amir Maftah
alipitisha krosi nzuri kwa Shomari Kapombe aliyepiga shuti kali
lililopaa juu ya lango la Mtibwa Sugar.
Katika dakika ya 18, pasi ya Barnabas ilimkuta
Ntebe aliyepiga shuti kali lililomshinda kipa Juma Kaseja na kujaa
wavuni hivyo kuipa Mtibwa Sugar bao la kuongoza.
Kuingia kwa bao hilo kuliamsha ari ya Mtibwa Sugar
kwani katika dakika ya 23, shuti la mshambuliaji Hussein Javu
lilipanguliwa kwa ustadi mkubwa na kipa Kaseja.
Simba ilijaribu kurudi mchezoni katika dakika ya
28, ambapo Felix Sunzu alipiga shuti kali, lakini lilipaa juu ya lango
la Mtibwa.
Katika mchezo huo kocha wa Simba, Liewig
hakuwaanzisha wachezaji wake mahiri, Amri Kiemba pamoja na Mrisho
Ngassa, lakini baadaye alifanya mabadiliko kwani aliwatoa Ramadhani
Chombo, Haruna Moshi na Haruna Chanongo na kuwaingiza Kigi Makasi,
Kiemba na Ngassa.
Katika hali ya kushangaza wachezaji Chombo na
Moshi baada ya kutolewa walikwenda moja kwa moja kwenye vyumba vya
kubadilishia nguo badala ya kukaa katika benchi.
0 comments:
Post a Comment