SEHEMU YA KWANZA.
Kwa ufupi
Tangu kuuawa kwa kiongozi wa Kundi la Al-Qaeda Osama
bin Laden kumekuwa na fununu nyingi zinazoeleeza mazingira ya kifo
chake pamoja na ujumla wa maisha yake wakati akiwa mafichoni.
TANGU kuuawa kwa kiongozi wa Kundi la Al-Qaeda Osama bin Laden
kumekuwa na fununu nyingi zinazoeleeza mazingira ya kifo chake pamoja na
ujumla wa maisha yake wakati akiwa mafichoni.
Katika mfulilizo wa makala haya, Mwandishi, GEORGE NJOGOPA makala iliyochapishwa gazeti la Mwananchi amepitia simulizi za askari aliyemuua kiongozi huyo kama alivyozungumza na mwandishi mmoja wa habari nchini Marekani.

Akiwa mtu mwenye tabasamu na ucheshi wa mbali,
askari (jina linahifadhiwa) anatoa maelekezo kwa mwandishi wa habari
aliyetaka kujua historia ya maisha yake jeshini.
Ndani ya mgahawa uliofurika watu waliochangamka kwa vinywaji, askari mwanamaji anaanza kueleza namna alivyojiunga na Jeshi la Wanamaji la Marekani hadi kufikia nafasi ya kuwa mlenga shahaba mkuu.
Ndani ya mgahawa uliofurika watu waliochangamka kwa vinywaji, askari mwanamaji anaanza kueleza namna alivyojiunga na Jeshi la Wanamaji la Marekani hadi kufikia nafasi ya kuwa mlenga shahaba mkuu.
Anasema anakumbuka kile kilichomsukuma kuchukua
uamuzi wa kujiunga na jeshi ni kama sehemu ya hasira iliyomkumba baada
ya kuachwa na mpenzi wake al iyedumu naye kwa kipindi kirefu.
“Unajua tukio la kuachwa na mpenzi wangu lilinivunja moyo sana… na ndiyo nikachukua uamuzi kwenda jeshini.
Anasema kuwa siku yake ya kwanza alipokwenda
kuomba kazi anakumbuka alimwambia ofisa mmoja wa jeshi kuwa alikuja hapo
kuomba kazi ya kulenga shahaba (sniper).
“Pale nilimkuta askari mfukuzi, mkufunzi
akaniuliza unataka nini… nikamwambia nataka kuwa mlenga shahaha, lakini
yeye akaniambia kuwa tayari walikuwa na walenga shabaha.
Hata hivyo alifaulu kuandikishwa na baadaye
kupelekwa kwenye mafunzo yaliyimwongezea ujuzi wa kazi na hatimaye
kuungana na vikosi vya wanajeshi wa maji vilivyosafiri sehemu mbalimbali
duniani.
Kama ilivyo kwa askari wengi wanamaji, askari huyu alishiriki kwenye operesheni mbalimbali za kijeshi ikiwemo zile zilizohusu katika nchi za Afghanistan na Iraq.
Kama ilivyo kwa askari wengi wanamaji, askari huyu alishiriki kwenye operesheni mbalimbali za kijeshi ikiwemo zile zilizohusu katika nchi za Afghanistan na Iraq.
Anasema operesheni yake kubwa ya kijeshi ilikuwa
nchini Afghanistan ambako vikosi vya Marekani vilivamia katika eneo hilo
katika kile kilichoelezwa na kukabiliana na utawala wa Taliban ambao
ulitajwa kuwa na ushirikiano wa karibu na Kundi la Kigaidi la Al-Qaeda.
“Uzoefu mkubwa wa kijeshi niliupata wakati nikiwa
Afghanistan ambako nakumbuka nilishiriki kikamilifu kukabiliana na
wanamgambo wa Taliban.
Tulipofaulu kuwafurusha wanamgambo hao tuliendelea kubakia nchini huko kuimarisha hali ya usalama na kusaidiana na wananchi wa eneo lile kurejesha hali ya usalama.
Tulipofaulu kuwafurusha wanamgambo hao tuliendelea kubakia nchini huko kuimarisha hali ya usalama na kusaidiana na wananchi wa eneo lile kurejesha hali ya usalama.
“Kichwa changu kilikuwa tayari kimeshazoea mizinga
na makombora, maana wakati mwingine umekaa sehemu ghafla unasikia
kombora linavurumishwa mbele yako… Ghala nyuma unasikia mlio wa
bunduki..
Kusema kweli nilijifunza mengi wakati nikiwa Afganistan.
Kusema kweli nilijifunza mengi wakati nikiwa Afganistan.
Wakati huo Marekani ilianzisha operesheni za
kukabiliana na Kundi la Al-Qaeda ambalo lililodaiwa kutekeleza tukio la
kigaida katika majengo yake mjini New York na Washington.
Shabaha ya Marekani ilikuwa kukabiliana na
kiongozi wa kundi hilo, Osama bin Laden ambaye wakati huo ilisemekana
amejichimbia mafichoni katika Milima ya Afghanistan.
SEHEMU YA PILI:
Kwa ufupi
“Unajua nilipomuua tu, baadaye askari wengi
walikuja. Kila mmoja alipiga risasi sehemu aliyojua yeye. Ndiyo maana
utakuta mwili wake ulikuwa na sehemu nyingi ziizopigwa risasi.
“Niliongeza risasi ya tatu, kisha nikamfuata yule mama nikamkalisha kitandani…kumbe pembeni kulikuwa na mtoto mwenye umri kati ya miaka miwili ama mitatu.
Huyu mtoto alikuwa wa Osama. Nilishtuka kidogo, nikamsogolea, maskini ya Mungu mtoto alilia kwa hofu na kutia huruma.
“Nilimchukua yule mtoto na kumweka kitandani kisha nikamnawisha maji na kuondoka kushuka chini kwa wenzangu”.
ALIYEKUWA kiongozi wa kundi la mtandao wa kigaidi la Al Qaeda,
Osama bin Laden aliuawa Mei Mosi, 2011 na vikosi vya Marekani
vilivyoyavamia maficho yake, Abbottabad, Pakistan.
Tukio la kuuawa kwa kiongozi huyo lilipokewa kwa shangwe kubwa duniani kote ikiwamo Marekani kwenyewe.
Tukio la kuuawa kwa kiongozi huyo lilipokewa kwa shangwe kubwa duniani kote ikiwamo Marekani kwenyewe.
Katika mfululizo wa simulizi hii askari aliyetekeleza mauaji hayo anaendelea kufahamisha jinsi alivyofanikisha operesheni hiyo.
Nyumba ya Osama bin Laden ilikuwa imezingirwa na
askari wa Marekani waliofika kwenye eneo hilo nyakati za usiku
wakiongozwa na rada maalumu iliyoratibiwa kutoka makao makuu ya jeshi,
Pentagon.
Wakati askari mlenga shabaha akiwa amepanda hadi ghorofa ya tatu, kulikuwa pia na askari wengine walioweka doria mlangoni.
Wakati askari mlenga shabaha akiwa amepanda hadi ghorofa ya tatu, kulikuwa pia na askari wengine walioweka doria mlangoni.
Alipofika ghorofa ya tatu, askari huyo alimkuta
Osama amesimama na mkewe huku wakiwa wamejihami kwa tukio lolote dhidi
yao.
Bila kupoteza muda askari huyo alimimina risasi mbili katika sehemu ya paji lake na ndipo Osama alipoanguka chini na kuaga dunia.
Aliongeza risasi nyingine katika sehemu ya mbavu zake na kisha akamsogelea mke wa Osama ambaye wakati huo alikuwa akilalama na kumtazama mumewe jinsi alivyokuwa akikata roho.
Bila kupoteza muda askari huyo alimimina risasi mbili katika sehemu ya paji lake na ndipo Osama alipoanguka chini na kuaga dunia.
Aliongeza risasi nyingine katika sehemu ya mbavu zake na kisha akamsogelea mke wa Osama ambaye wakati huo alikuwa akilalama na kumtazama mumewe jinsi alivyokuwa akikata roho.
“Niliongeza risasi ya tatu, kisha nikamfuata yule mama nikamkalisha kitandani…kumbe pembeni kulikuwa na mtoto mwenye umri kati ya miaka miwili ama mitatu.
Huyu mtoto alikuwa wa Osama. Nilishtuka kidogo, nikamsogolea, maskini ya Mungu mtoto alilia kwa hofu na kutia huruma.
“Nilimchukua yule mtoto na kumweka kitandani kisha nikamnawisha maji na kuondoka kushuka chini kwa wenzangu”.
Anasema tukio hilo lilichukua sekunde 15.
Wakiwa bado wameshikwa na bumbuwazi baadhi ya askari walifika chumbani kwa Osama na kuukuta mwili wake ukiwa sakafuni.
Pamoja na kwamba Osama alikuwa tayari amekwishafariki dunia, bado askari hao waliumiminia tena risasi mwili wa Osama na kisha baadaye waliushusha hadi chini na kuufunga katika mfuko maalumu.

Kisha waliendelea na kazi ya upekuzi ili kubaini
kama kulikuwa na vitu vingine ambavyo Osama alikuwa akitumia kufanikisha
maficho yake. Anasema kuwa walibaini vitu vingi zikiwamo kompyuta
zilizowekwa katika kila chumba.
Waliziharibu kompyuta hizo na kuchukua taarifa walizoona kwao ni muhimu.
Waliziharibu kompyuta hizo na kuchukua taarifa walizoona kwao ni muhimu.
“Lakini tulistaajabu kweli, maana kila chumba tulichoingia tulikuta kompyuta.”
Askari hao pia walibaini vifaa maalumu vilivyowekwa chini ya kitanda ambavyo hata hivyo taarifa zake hazikutolewa mara moja kama vifaa hivyo vilitumika kwa nini.
Askari hao pia walibaini vifaa maalumu vilivyowekwa chini ya kitanda ambavyo hata hivyo taarifa zake hazikutolewa mara moja kama vifaa hivyo vilitumika kwa nini.
“Ndani ya nyumba ile kulikuwa na mambo mengi,
maana pamoja na kushuhudia vifaa vya kunasia mawimbi ya sauti lakini
kulikuwa na hifadhi kubwa ya chakula.
Binafsi pia nilikuta lundo la dawa za kulevya aina ya Opium ambazo nadhani alikuwa akitumia Osama ama wafuasi wake maana tulizikuta katika vyumba vya chini.”
Binafsi pia nilikuta lundo la dawa za kulevya aina ya Opium ambazo nadhani alikuwa akitumia Osama ama wafuasi wake maana tulizikuta katika vyumba vya chini.”
Baada ya operesheni ya kuikagua nyumba hiyo
kukamilika, askari hao wakiwa na msafara wao walirejea hadi ilikokuwa
kambi ya vikosi vya Marekani mjini Jalalabad kwa ajili ya kuwasilisha
mwili wa Osama bin Laden pamoja na familia yake.
Mkuu wa ngome ya Jalalabad alipewa taarifa ya operesheni hiyo na baadaye alifanya utambuzi kwa mwili wa Osama kabla ya kutoa taarifa yake ya mwisho makao makuu Washington.
Mkuu wa ngome ya Jalalabad alipewa taarifa ya operesheni hiyo na baadaye alifanya utambuzi kwa mwili wa Osama kabla ya kutoa taarifa yake ya mwisho makao makuu Washington.
Kamanda McRaven akiwa na ofisa wa CIA walichukua
vipimo vya mwili wa Osama na kujiridhisha kuwa ndiye yeye aliyeuawa.
Wakati wanachunguza waliona matundu mengi ya risasi katika sehemu za
kifua hadi miguuni.
“Unajua nilipomuua tu, baadaye askari wengi
walikuja. Kila mmoja alipiga risasi sehemu aliyojua yeye. Ndiyo maana
utakuta mwili wake ulikuwa na sehemu nyingi ziizopigwa risasi.
SEHEMU YA TATU:
Kwa ufupi
“Wakati nikiwa Jalalabad niliwaambia watoto wangu
kutosema chochote kwa marafiki zao kuhusiana na kazi yangu hasa baada ya
kujulikana kuwa mimi ndiye niliyemuua Osama.
MAREKANI inaamini kuwa vita vya kukabiliana na ugaidi vimepata mafanikio baada ya kuuawa kwa kiongozi wa kundi la Al-Qaeda, Osama bin Laden aliyeuawa Mosi, 2011 nchini Pakistan.
MAREKANI inaamini kuwa vita vya kukabiliana na ugaidi vimepata mafanikio baada ya kuuawa kwa kiongozi wa kundi la Al-Qaeda, Osama bin Laden aliyeuawa Mosi, 2011 nchini Pakistan.
Hivi karibuni askari aliyefyatua risasi na kumuua
kiongozi huyo alifanya mahojiano na mwandishi mmoja wa habari kuelezea
namna operesheni hiyo ilivyofanikiwa.
Katika mfululizo wa simulizi hiyo leo mwandishi
George Njogopa anapitia sehemu ya mwisho ambayo inamulika upande wa
maisha yake binafsi.
Kulikuwa na furaha na shangwe kila kona ya Marekani na duniani kote. Mhalifu wa kimataifa alikuwa ameondoshwa kwenye uso wa dunia.
Kulikuwa na furaha na shangwe kila kona ya Marekani na duniani kote. Mhalifu wa kimataifa alikuwa ameondoshwa kwenye uso wa dunia.
Askari aliyefyatua risasi na kumaliza uhai wa Osama alikuwa tayari amerejea nyumbani.
Rais Barack Obama aliingia kwenye rekodi mpya kwa kuwa kiongozi aliyefanikisha kuangusha ngome muhimu ya mtandao wa Al-Qaeda.
Rais Barack Obama aliingia kwenye rekodi mpya kwa kuwa kiongozi aliyefanikisha kuangusha ngome muhimu ya mtandao wa Al-Qaeda.
Baadhi ya askari wa Marekani waliopiga kambi
katika mji wa Jalalabad nchini Pakistan waliambatana na askari mlenga
shabaha kurejea nyumbani.
Askari huyo anasema kuwa, “Tulivyomaliza
operesheni yetu tukarejea nyumbani kuendelea na majukumu mengine.
Nakumbuka nilivyoondoka Jalalabad nilirejea moja kwa moja kwenye kituo cha vikosi vya majini na kuendelea na shughuli nilizopangiwa.”
Nakumbuka nilivyoondoka Jalalabad nilirejea moja kwa moja kwenye kituo cha vikosi vya majini na kuendelea na shughuli nilizopangiwa.”
Askari huyu ambaye ndiye aliyekuwa mtu wa mwisho
kumwona Osama wakati akiwa hai kabla hajammiminia risasi mbili za usoni
amesema sasa anaishi maisha ya upweke tofauti na miaka ya nyuma.
Anasema kuwa wakati akiwa katika operesheni nchini
Pakistan mkewe pamoja na watoto wake waliishi maisha ya mahangaiko na
wakati mwingine walilazimika kuhama mji mmoja hadi mwingine wakihofia
pengine wangevamiwa na makundi yenye uhusiano na vikundi vya kigaidi.
“Wakati nikiwa Jalalabad niliwaambia watoto wangu
kutosema chochote kwa marafiki zao kuhusiana na kazi yangu hasa baada ya
kujulikana kuwa mimi ndiye niliyemuua Osama.
Nakumbuka wakati fulani mke wangu aliwafuata
maofisa wa CIA akitaka kubadilisha jina na apelekwe katika mji mwingine
kwa hofu kuwa pengine angevamiwa na watu wasiojulikana.
Hata hivyo jaribio lake hilo halikufaulu na
baadaye akaamua kuondoka na kwenda kuishi katika mji mwingine akiwa na
watoto.
Askari huyo anasema kuwa muda mwingi aliotumia jeshini ulimfanya apoteze upendo wa karibu na familia yake jambo lililosababisha kuvunjika kwa ndoa yake.
Askari huyo anasema kuwa muda mwingi aliotumia jeshini ulimfanya apoteze upendo wa karibu na familia yake jambo lililosababisha kuvunjika kwa ndoa yake.
Wakati akizungumza katika mahojiano maalumu na
mwandishi mmoja wa habari, mke wa askari huyo alieleza sababu za
kuachana na mumewe ambaye alikuwa ameishi naye kwa zaidi miaka 10.
“Sikupenda kuendelea kuishi maisha ya hofu… halafu isitoshe muda mwingi nilikuwa mpweke na mwenzangu mara zote alikuwa kwenye safari za mbali.
“Sikupenda kuendelea kuishi maisha ya hofu… halafu isitoshe muda mwingi nilikuwa mpweke na mwenzangu mara zote alikuwa kwenye safari za mbali.
0 comments:
Post a Comment