Kwa ufupi:
MATOKEO mabaya ya mtihani wa kidato cha nne yamezidi
kuibua mapya, baada ya wamiliki wa shule na vyuo binafsi nchini kusema
mitihani ilitungwa kwa mfumo tofauti na uliozoeleka miaka yote, huku
tume iliyounndwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ikipondwa na baadhi ya
watu.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk Shukuru Kawambwa akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam.
.
MATOKEO mabaya ya mtihani wa kidato cha nne yamezidi kuibua
mapya, baada ya wamiliki wa shule na vyuo binafsi nchini kusema mitihani
ilitungwa kwa mfumo tofauti na uliozoeleka miaka yote, huku tume
iliyounndwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ikipondwa na baadhi ya watu.
Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Shule na Vyuo
Binafsi nchini (TAMONGSCO), Mahmoud Mringo alisema kwamba maswali
waliyoulizwa watahiniwa yalikuwa ya kujieleza tofauti na miaka ya nyuma,
ambapo mfumo uliotumika uliwataka watahiniwa kutaja vitu tu bila ya
kulazimika kuvielezea kwa undani.
Kauli yake iliungwa mkono na Mkuu wa Taaluma
katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Marian, Florence Mapunda
ambaye alisema kuwa mtihani wa mwaka jana ulitaka zaidi watoto kujieleza
tofauti na miaka ya nyuma wakati wanafunzi walipokuwa wanakariri.
Hata hivyo, Msemaji wa Baraza la Mitihani Tanzania
(Necta), John Nchimbi alisema mfumo wa mtihani haukubadilika kwa namna
yoyote na kuwa upo kama ule wa miaka yote.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip
Mulugo, kwa upande wake alisema madai yanayotolewa hayana msingi, huku
akihoji kwa nini yasitoke tangu mitihani ilipokuwa ikifanyika na badala
yake yanatoka baada ya kutangazwa kwa matokeo.
Matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika
mwaka jana yanaonyesha kuwa watahiniwa 240,903 sawa na asilimia 60.6
wamepata sifuri, huku wanafunzi 23,520 tu ambao ni sawa na asilimia 5.16
ndiyo waliofaulu na wengine 103,327 sawa na asilimia 26.02 wamepata
daraja la nne.
Kutokana na matokeo hayo, Waziri Mkuu Pinda, juzi
alitangaza kuunda tume ya kuchunguza chanzo cha matokeo hayo kuwa
mabaya, hatua ambayo hata hivyo imekosolewa na wasomi wa Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam (UDSM).
Tume hiyo inayoundwa na wajumbe kutoka Taasisi za
Elimu, Chama cha Waalimu, Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii na Umoja wa
Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (Tahossa) inatarajiwa kuanza kazi
wiki hii.
Profesa Gaudence Mpangala wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam alisema kuunda tume ni kupoteza muda kwa sababu matatizo na
changamoto zote ndani ya sekta hiyo yanajulikana, huku mwenzake, Profesa
Chriss Maina pia wa UDSM akisema kuunda tume hakutaisaidia kwa kuwa
Serikali inaidharau sekta ya elimu.
“Tatizo ni kutowekeza kikamilifu katika sekta ya
elimu, imekuwa na matumizi makubwa katika mambo yasiyokuwa ya
lazima,”alisema Profesa Mpangala.
Alisema matatizo mengine ni mazingira magumu ya
kufundisha na uhaba wa walimu.
“Kinachotakiwa wajipange kufanyia kazi changamoto hizi zilizopo badala ya kuunda tume, wakati fedha nyingi tunasikia inapotea kwenye ubadhirifu,”alisema Profesa Mpangala.
“Kinachotakiwa wajipange kufanyia kazi changamoto hizi zilizopo badala ya kuunda tume, wakati fedha nyingi tunasikia inapotea kwenye ubadhirifu,”alisema Profesa Mpangala.
Naye Profesa Maina alisema:
“Hiyo tume ya kazi gani kwa sababu matatizo yanafahamika wazi, umewahi kusikia taifa gani ambalo halina mtalaa wa elimu. Hiyo ndiyo hali halisi kwa nchi yetu.”.
“Hiyo tume ya kazi gani kwa sababu matatizo yanafahamika wazi, umewahi kusikia taifa gani ambalo halina mtalaa wa elimu. Hiyo ndiyo hali halisi kwa nchi yetu.”.
0 comments:
Post a Comment