Kwa ufupi
Kazi ya kuhesabu upya kura za urais kutoka
vituo vya kupigia kura 22 ilianza mapema jana chini ya ulinzi mkali
baada wa mawakala wa Muungano wa Cord na Jubilee kuapishwa.
http://www.mwananchi.co.tz
RAILA ODINGA AKIPIGA KURA KATIKA UCHAGUZI MKUU WA KENYA.
UHURU KENYATTA AKIPIGA KURA KATIKA UCHAGUZI MKUU WA KENYA.
NAIROBI. MAHAKAMA ya Juu (Supreme Court) nchini Kenya jana ilitupilia mbali viapo viwili katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Uhuru Kenyatta wa Muungano wa Jubilee.
Maombi yaliyotupwa ni lile la muungano wa
mashirika yasiyo ya kiserikali lililoitaka mahakama iamuru tume ya
uchaguzi kufikisha mahakamani hapo nyaraka zote zilizotumika wakati wa
uchaguzi huo.
Kadhalika mahakama hiyo ilitupilia mbali hati ya
kiapo yenye kurasa 839 kilichowasilishwa na upande wa Muungano wa Cord
ambacho kilidai kwamba kura katika majimbo 120 zilikuwa haziwiani na
idadi ya wapigakura, hivyo kuitaka mahakama hiyo iitishe uchunguzi wa
kina kwa daftari hilo pamoja na kura zilizopigwa.
Katika kiapo cha Cord, Jaji Phillip Tunoi alisema
kwa mujibu wa sheria hati za kiapo si haki ya mlalamikaji au mlalamikiwa
hivyo kabla wa kuwakilishwa walalamikaji walipaswa kupata ruhusa ya
mahakama, jambo ambalo halikufuatwa.
Kwa upande wake Jaji Mohammed Warsame aliyesoma
uamuzi dhidi ya kiapo cha mashirika yasiyokuwa ya kiserikali alitupilia
mbali maombi yao kwa maelezo kwamba yalifikishwa mahakamani nje ya muda
uliowekwa kisheria.
Katika ombi lao muungano huo wa Africog ulidai
kuwa kufeli kwa mfumo wa kielectronikiwa kuhesabu kura ulikuwa umepangwa
kwa madhumuni ya kuiba kura. Hivyo tume hiyo iamuriwe kuleta mahakamani
hapo nyaraka zote ili zifanyiwe uchunguzi wa kitaalamu.
0 comments:
Post a Comment