Kwa ufupi
Majosho yanayofanya kazi yapo kwenye Vijiji vya Dirma, Dawar, Gitting, Mureru na Gendabi. Dk Tom Maeda.
Yadaiwa magonjwa yote yanaambukizwa na kupe kutokana na kukosa majosho.
HANANG.
ZAIDI ya mifugo 5,000 huugua na 600 kati ya hiyo hufa kila mwaka kutokana na maradhi yaletwayo na kupe, ilielezwa.
ZAIDI ya mifugo 5,000 huugua na 600 kati ya hiyo hufa kila mwaka kutokana na maradhi yaletwayo na kupe, ilielezwa.
Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo
walisema hayo kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo, yaliyoandaliwa na
asasi isiyo ya kiserikali ya nchini Uholanzi ya (SNV) na Ofisi ya Waziri
Mkuu Tamisemi.
Madiwani hao waliazimia kutoa msukumo kwa
jamii,ili majosho yaliyoharibika wayatumie pindi yakitengenezwa,kwani
kati ya majosho 21 ni sita yaliyo na hali nzuri, 10 yanahitaji
matengenezo na manne yanahitaji kujengwa upya.
Madiwani hao walidai kuwa wenyewe ndiyo
wanapitisha bajeti ya halmashauri ya wilaya hiyo, hivyo wapo tayari
kuidhinisha kwenye bajeti zao fedha za kuboresha majosho na ununuzi wa
dawa za kuogeshea mifugo.
Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya
ya Hanang’ Felix Mabula alisema wilaya hiyo ni miongoni mwa wilaya
zenye mifugo mingi mkoani Manyara na inaingiza mapato mengi hivyo ni
wajibu kuijengea mazingira bora.
“Kwa vile madiwani wamejengewa uwezo wa kutambua
madhara ya kutoogesha mifugo, naamini wataufikisha ujumbe huu kwa jamii
ya maeneo yao ili zoezi la kuogesha mifugo lianze kwenye majosho yote,”
alisema Mabula.
Kwa upande wake, Ofisa mifugo na uvuvi wa
halmashauri ya wilaya hiyo, Dk Tom Maeda alisema majosho yanayofanya
kazi yapo kwenye Vijiji vya Dirma, Dawar, Gitting, Mureru na Gendabi.
0 comments:
Post a Comment