RAIS wa Kenya Uhuru Kenyatta (kushoto) akiwa na Makamu wa Rais William Ruto wakati wa kutangaza majina ya Mawziri wapya.
Rais wa
Kenya Uhuru Kenyatta akishirikiana na Makamu wa Rais William Ruto
ametangaza kwa mara ya pili majina 12 ya Mawaziri watakaounda Baraza
jipya.
Orodha
imefanya idadi ya Mawaziri hao walioteuliwa kufikia Mawaziri 16 huku
wananchi wakiendelea kusubiri nafasi mbili kwani awali Rais Kenyatta
aliutangazi umma kuwa baraza lake la mawaziri litakuwa na watu 18 tu.
Miongoni
mwa mawaziri walioteuliwa na wizara zao zikiwa kwenye mabano ni Najib
Balala( Madini ), Charity Ngilu (Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya mijini ),
Adan Mohamed ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji
wa Benki ya Baclays Afrika (Viwanda na Maendeleo ya Biashara).
Wengine
ni Anne Waiguru(Maendeleo ya wananchi na Mipango), Felix Tarus
Kosgey(Kilimo, Mifugo na Uvuvi), Judy Wahungu(Maji na Maliasili), Hassan
Wario(Michezo na Utamaduni), Jacob Kaimenyi (Elimu) Francis Kimemia
(Katibu wa Baraza la Mawaziri) na Lawrence Lenayapa (Mnadhimu wa
Ikulu).
0 comments:
Post a Comment