NITAOMBA niende na Waziri (Profesa Jumanne Maghembe)
au naibu wake (Dk Binilith Mahenge) ili wakawaeleze wananchi wa
Morogoro ni lini watawapatia maji kwa kuwa wamechoshwa na visima hivi
mdundiko,”
Mchungaji Lwakatare.
Dodoma. Ni kilio kila kona. Hivi ndivyo
unavyoweza kuuelezea mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji
uliowasilishwa bungeni mjini Dodoma jana.
Vilio hivyo vya wabunge waliochangia mjadala huo
ndivyo vilivyomfanya mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Mchungaji Dk Getrude
Lwakatare alieleze bunge kuwa wananchi wa Mkoa wa Morogoro, hususan maeneo ya
Ifakara na Kilombero wamechoshwa na ukosefu wa maji ambao umewakumba kwa muda
mrefu.
Dk Lwakatare akaeleza kuwa wananchi hao wameishi kwa miaka mingi na
uhaba huo, wakitegemea visima vya kusukuma, maarufu kama visima mdundiko na
kuitaka Serikali ihakikishe inawapatia ufumbuzi wa kero ya maji.
Katika mchango wake, Mchungaji Rwakatare
alisema kuwa wanawake na watoto wa Ifakara na Kilombero wamekuwa
katika wakati mgumu kutokana na kukosekana kwa maji licha ya kuishi jirani na
mito inayotiririsha maji kwa muda wote.
“Ni lazima Serikali ihakikishe
katika bajeti ya mwaka huu inawapatia wananchi hao maji, wamechoshwa na visima
hivi mdundiko.
Nitaomba niende na Waziri (Profesa Jumanne Maghembe)
au naibu wake (Dk Binilith Mahenge) ili wakawaeleze wananchi wa
Morogoro ni lini watawapatia maji kwa kuwa wamechoshwa na visima hivi
mdundiko,”alisema Mchungaji Lwakatare.
Aliongeza kuwa kuna kila sababu ya
kuhakikisha wananchi wanapata maji kwa kuwa ni wajibu wa Serikali kufanya
hivyo. Mbali na Lwakatare, Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Muhonga
Said Ruhwanya aliililia Serikali na kuomba iwasaidie wananchi
mkoani Kigoma kupata maji kwa kuwa maji ni uhai ambao kila mtu anahitaji.
“Kule Kigoma kuna vijiji havina maji tunaomba
mvisaidie muwasaidie na watu wa Mwandiga ili waweze kupata maji kwa
haraka,”alisema.
Naye Mbunge wa Moshi Vijijini(CCM), Dk Cyril Chami
aliwataka wabunge kuacha kumlalamikia Waziri wa Maji na Umwagiliaji na badala
yake alisema ni muhimu wakakaa chini na kufanya uamuzi kwa pamoja.
“Hakuna cha kumlaumu waziri hapa, wabunge tuache
kulalamika, tukae chini tufanye maamuzi ambayo tunayahitaji,”alisema Dk Chami
na kuongeza: “Kuna kiongozi mmoja hapa nchini amekuwa akisema tunahitajika
kufanya maamuzi magumu hivyo tufanye.”
0 comments:
Post a Comment