BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

NAOMBA KATIKA HILI LA MTOTO HUYU TUUNGANE KUMSAIDIA

9 986b1KIUKWELI inasikitisha sana kwa Madaktari wa HOSPITALI YA GENERAL iliyoko mjini Dodoma kutomtibu mtoto Ombeni Mbeula kwa takribani miezi miwili kwa ukosefu wa pesa kutoka kwa familia yake. 
Isitoshe mtoto mwenyewe ana miaka mitano (5) inabidi kiutaratibu apate matibabu bure, hivi kweli uongozi wa hospitali ya General umelisimamiaje jambo hili?. 
Kiukweli inasikitisha kwa madaktari kutomjali mtoto Ombeni Mbeula mpaka habari iliporushwa kwenye mtandao  na washiriki wake wa blog nyingine ndipo madaktari walipoanza kuitwa lakini hawajaenda kumtibu mtoto huyo.

Kwa moyo wa dhati tunawashukuru wale wote waliotoa michango yao kupitia kupitia kwenye namba ya ndugu yake ambayo ni Ekiria Paskali na namba yake ya simu ni
 0757  498 336.

Hawa ni baadhi ya wale walioguswa na tukio hilo na kutoa mchango wao wa hali na mali jumla ya michango ni shilingi 421,300 mpaka naondoka hospitalini hapo kuna watu walikuwa bado wanaendelea kuchangia. 
Kama ulikuwa unataka kumchangia mtoto huyu apate matibabu tuma mchango wako kwa kutumia namba hii 0757 498336 mwenye jina lake ni Ekiria Paskali.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: