MATUKIO YA AFRIKA.
RAIS wa Kenya, Uhuru Kenyatta, yuko katika harakati ya kuunda serikali
yake kwa kuanza kutaja majina ya mawaziri wanne kati ya mawaziri 18
watakaokuwepo katika baraza lake la mawaziri.Baraza la mawaziri nchini Kenya awali lilijumuisha mawaziri 44.
Hapo jana Rais huyo mpya aliyechaguliwa katika uchaguzi uliofanyika Machi 4 nchini humo, alimteau mwanadiplomasia Amina Mohammed kuwa waziri wa mambo ya nchi za nje.
Amina ambaye ni mwanamke wa kwanza kuteuliwa katika nafasi hiyo tangu Kenya ijinyakulie Uhuru wake mnamo mwaka wa 1963, alianza taaluma yake katika wizara hiyo kisha akajiendeleza kupitia wizara ya sheria.
Kabla ya kujiunga na Umoja wa Mataifa, Amina alikuwa akiwania nafasi ya Pascal Lamy ya kuwa mkurugenzi mkuu wa shirika la biashara duniani, WTO, kabla ya kuchujwa katika nafasi hiyo mapema mwezi huu.
Rotich ambaye ni msomi na mchumi alifanya kazi kwa muda mrefu katika wizara ya fedha nchini Kenya na hata katika Benki kuu ya nchi hiyo.
Mawaziri wengine wawili walioteuliwa hapo jana ni pamoja na waziri wa Mawasiliano Daktari Fred Okeng'o Matiangi na waziri wa Afya Bwana James Wanaina Macharia.
Rais Uhuru Kenyatta amesema mawaziri wengine 14 watatajwa baadaye. Rais Uhuru hakutaja tarehe kamili ya kutangaza majina hayo.
Kamati ya bunge kuwachuja mawaziri wateule.
Hata hivyo kabla wanne hao walioteuliwa kuthibitishwa kuwa mawaziri kamili ni lazima wapitie mchujo katika kamati ya bunge inayoongozwa na Spika wa Bunge, Justin Muturi.
Kulingana na katiba ya Kenya ni lazima majina ya maafisa wakuu wa serikali, wakiwemo mawaziri, mabalozi na wakuu wa tume za kikatiba, wapitishwe na kamati ya bunge.
Huku hayo yakiarifiwa wataalamu nchini Kenya wanasema huenda mawaziri walioteuliwa hapo jana wakapitishwa bila pingamizi lolote kutokana na kamati hiyo ya bunge iliyoteuliwa kufanya mchunjo huo kujumuisha wabunge 16 wa muungano wa Jubilee wake Uhuru Kenyatta na wabunge 10 kutoka kwa muungano wa Cord. Kamati hiyo pia ina mwanachama mmoja ambaye haegemei upande wowote.
Rais Kenyatta aahidi kuinua uchumi wa nchi
Rais Uhuru Kenyatta awali aliahidi kuimarisha marudufu uchumi wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki na kuwaondoa katika umaskini Wakenya milioni 10 kati ya milioni 40 idadi ya raia wa nchi hiyo ifikapo mwaka wa 2017.
Katika Ghasia hizo pia watu wengi waliachwa bila makaazi nchini humo.

0 comments:
Post a Comment