BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS WA ZANZIBAR DK SHEIN: SIONGOZI ZANZIBAR KWA MATAKWA YA MTU.

SheinRais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein.
RAIS wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, amesema hatoongoza serikali yake kwa shikinikizo la mtu au kiongozi yeyote.
Aidha, amewashangaa wanaohoji sababu za yeye kutowateua wakuu wa wilaya na mikoa wapya tangu achaguliwe kuwa Rais mwaka 2010.
 
Rais Shein aliyasema hayo wakati akiwahutubia wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara uliofanyika Amani Mkoa wa Mji Unguja.
 
Alisema kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, yeye ndiye Rais baada ya kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na ndiye aliyewateua Makamu wa Kwanza na wa Pili wa Rais kuwa wasaidizi na washauri wake.
 
Aidha, alisema kutokana na nguvu za kikatiba na kisheria alizonazo, anaweza kumuondoa yeyote katika uteuzi wake bila ya kuvunja na kikuika sheria ikiwa hataridhishwa na utendaji wa kiongozi aliyemteua.
 
Kauli ya Dk. Shein, ilionekana ni kama kumpiga `kijembe' Makamu wake wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad, ambaye aliwahi kutamka katika mkutano wa hadhara Fuoni katika uwanja wa Magirisi kuwa hawezi kufukuzwa kazi na Rais.
 
“Mimi ndiye mshindi wa urais wa Zanzibar mwaka 2010, nimeunda serikali na kuteua Makamu wa Kwanza na wa Pili ili kunisaidia kazi na kunipa ushauri, nimetengeneza wizara na kuteua mawaziri na naibu mawaziri bila ya kupangiwa na mtu na wakati wowote naweza kumuondoa yeyote,” alisisitiza.
 
Tangu kuchaguliwa kwake, Dk. Shein ameendelea kubakia na wakuu wa mikoa na wilaya wale wale aliowateua Rais wa awamu ya sita, Amani Abeid Karume na kufanya mabadiliko madogo katika Wilaya ya Kati na Kaskazini `B’ kati ya wilaya 10 za Unguja na Pemba.
 
Kutowateua wakuu wa wilaya na mikoa, kumewahi kuhojiwa mara kadhaa na baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kwa nyakati tofauti wakiwa kwenye vikao vya Baraza. 
 
Rais Dk. Shein alisema ana uzoefu na maarifa ya kutosha katika masuala ya uongozi na anapenda kuheshimu Katiba na kufuata sheria na hapendi kukurupuka au kusema kutokana na watu wanavyosema mitaani na kwenye majukwaa ya kisiasa.
CHANZO: NIPASHE
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: