PSPF YAELEZA ILIVYOFILISIWA KWA DENI LA TRIONI 6/-
http://www.freemedia.co.tzNaibu Waziri wa Fedha, Janeth Mbene.
SERIKALI imekiri kuhusika kuufilisi Mfuko wa Pensheni kwa
Watumishi wa Umma (PSPF) kutokana na kushindwa kulipa zaidi ya sh
trilioni 6.4 inazodaiwa.
Fedha hizo zinatokana na malimbikizo ya madeni sugu na ya muda mrefu ya fedha za PSPF zilizokopwa na baadhi ya taasisi, zikiwamo za umma kwa kudhaminiwa na serikali.
Hatua hiyo ilibainika jana wakati Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC) ilipokutana
na uongozi wa PSPF na uiagiza serikali kuhakikisha inaanza kulipa madeni hayo na taarifa ya utekelezaji wa agizo hilo kupelekwa mara moja kwenye kamati hiyo ndani ya wiki hii.
PAC chini ya mwenyekiti wake Zitto Kabwe ilikutana na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), uongozi wa PSPF, Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) na Wizara ya Fedha, kutaka kupata picha halisi ya tatizo la mfuko huo.
Kamati hiyo ambayo imetoa wiki moja kwa serikali kuja na majibu imelazimika kuingilia kati kunusuru mfuko huo ambao umeelezwa kwamba umefilisika kutokana na uwezo wake wa kuwalipa wastaafu mafao yao kushuka kwa kiwango cha kutisha.
Uwezo wa PSPF wa kuwalipa wastaafu hao mafao yao umeelezwa kuwa umeshuka kufikia asilimia 10 badala ya asilimia 40, kutokana na upungufu wa thamani ya mfuko huo unaofikia sh trilioni 6.4 hadi sasa.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu alikieleza kikao hicho kuwa kama malimbikizo ya madeni hayo hayatalipwa ndani ya kipindi cha miaka mitatu kuanzia sasa, mfuko huo utakabiliwa na hatari ya kufilisika kabisa.
Mayingu alisema malimbikizo ya madeni hayo yalianza baada ya serikali kushindwa kulipa sh bilioni 250.
Alisema fedha hizo zilitakiwa zilipwe na serikali baada ya kuwaingiza watumishi wake kwenye mfuko huo ulipoanzishwa mwaka 1999.
Mayingu aliendelea kuianika serikali kuwa kabla ya PSPF kuanzishwa, watumishi wa umma wastaafu walikuwa wakilipwa fedha za mafao yao kupitia Hazina.
Alisema kikosi kazi kilichoundwa na serikali mwaka 1997, kilifanya tathmini na kubaini kwamba kama serikali isingekuwa imelipa fedha hizo sh bilioni 250 kufikia mwaka 2006, upungufu wa thamani ya fedha za PSPF ungefikia sh bilioni 658.
Mayingu alisema pia mwaka 2003 ilifanyika tathmini nyingine na kubaini upungufu wa thamani ya fedha za PSPF za kuwalipa wastaafu ni sh bilioni 933.4.
Vilevile alisema tathmini nyingine ilifanyika mwaka 2007 na kubaini upungufu wa thamani ya fedha za mfuko huo za kuwalipa wastaafu sh trilioni 3.3.
Alisema kutokana na upungufu huo, uwezo wa PSPF wa kuwalipa wastaafu kipindi hicho ulishuka kutoka asilimia 93 hadi asilimia 43 na sasa umefikia kumi.
Mayingu alisema kutokana na malimbikizo ya madeni hayo, hivi sasa upungufu wa thamani ya fedha za mfuko huo za kuwalipa wastaafu umefikia sh trilioni 6.4.
“Thamani ya sasa ya kuwalipa wastaafu ni sh trilioni 6.4. wanachama wanaongezeka, muda unaongezeka na nakisi (upungufu) inakwenda, inakua.
Tunaweza kufikia mahali tukashindwa kulipa,” alisema.
Alisema hali hiyo inatokana na uwezo wa PSPF wa kuwalipa wastaafu hivi sasa kushuka kutoka asilimia 93 hadi asilimia 10.
Kutokana na hali hiyo, alionya kuwa kama malimbikizo ya madeni hayo hayatalipwa ndani ya kipindi cha miaka mitatu kuanzia sasa, mfuko huo utakabiliwa na hatari ya kufilisika kabisa.
Alisema kuanzia mwaka 2010, serikali ilichukua dhima ya kulipa sh bilioni 71, lakini hadi sasa haijalipa sh bilioni 716.
“Ukishaonesha kushindwa kuwalipa watumishi imani itawavunjika,” alionya Mayingu.
Alishauri kwamba pamoja na kulipa malimbikizo ya madeni hayo, serikali pia inapaswa kuongeza michango kutoka asilimia 15 za sasa hadi asilimia 25 ili kufidia upungufu uliopo.
Katika maagizo ya PAC, waliitaka serikali kulipa fedha hizo kwa kuanza kutoa sh bilioni 50 kwa mfuko huo.
Pili kamati hiyo imetoa siku saba kwa serikali kuja na majibu kamili baada ya jana kudai kuwa hawakujiandaa.
Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Irene Isaka alisema kulingana na tathmini waliyoifanya, wamebaini kuwa PSPF ina hali mbaya.
Alisema kutokana na hali hiyo, Machi mwaka huu, walitoa mwongozo, ikiwamo kutaka wanachama wa mfuko huo kutolipwa kiasi chote, bali kile tu walichochangia.
Irene alisema mbali na mwongozo huo, pia wanashauri pamoja na mambo mengine, serikali kulipa sh trilioni 1.2 ambazo ni sawa na asilimia 70 ya malimbikizo ya madeni kufidia upungufu wa thamani ya fedha za PSPF za kuwalipa wastaafu mafao yao.
Naibu Waziri wa Fedha, Janeth Mbene alisema wanakubali kwa asilimia 100 kwamba PSPF inaidai serikali.
Hata hivyo, alisema kwa sasa serikali haiwezi kutoa kiasi hicho cha fedha kwani kinaweza kuathiri mipango mingine ya maendeleo.
“Itabidi tujipange upya na kuanzia sasa kipaumbele cha serikali itakuwa ni kurejesha fedha hizo. Kwa mwaka huu tutatoa sh bilioni 50,” alisema.

0 comments:
Post a Comment