Daktari wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro, Alex Magufwa akimchunguza mtoto, Razaki Ramadhani (5) katika wodi ya watoto ya hospitali hiyo baada ya mtoto huyo kulazwa kwa ugonjwa wa malaria ikiwani ni siku ya maadhimisho ya siku ya malaria duniani inayoadhimishwa April 25 kila mwaka, Hospitali ya mkoa wa Morogoro ni miongoni mwa hospitali zinazopokea idadi kubwa ya wagonjwa wa malaria.
Picha JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
DKT MAGUFWA HAPA AKIENDELEA NA UCHUNGUZI KWA MTOTO IDDY AMRI (1) KWENYE WORI HIYO.
DKT ALEX MAGUFWA AKIMCHUNGUZA MTOTO BILAL GANDA KATIKA WODI HIYO.MTOTO ANAYESUMBULIWA NA UGONJWA WA MALARI.
TANZANIA inakadiriwa kwamba kuna vifo 60,000-80,000 kila mwaka vinavyotokana na malaria huku taifa likipoteza 3.4% ya mapato yake kutokana na kuhudumia ugonjwa wa malaria ambapo lengo kuu ni kupunguza kwa asilimia 50, idadi ya wagonjwa wa malaria na idadi ya vifo.
Lengo la kauli mbiyo ya mwaka huu "kupata maendeleo na mafanikio" ni kutokomeza vifo kutokana na malaria ifikapo 2015.
SHIRIKA la Afya Duniani, WHO, inaripoti kwamba mwaka 2009 takriban
watu bilioni 3.3, ikiwa ni nusu ya wakazi wote duniani, walikabiliwa na
hatari ya kuambukizwa na malaria. Kila mwaka hiyo inapelekea watu milioni 250 kuugua homa ya malaria na kusababisha karibu vifo elfu 850.
Mkutano mkuu wa 60 wa Shirika la Afya Duniani ulizindua rasmi siku ya malaria duniani mwaka 2007 kuadhimisha juhudi duniani za kudhibiti ugonjwa wa Malaria.
Siku hii ni ya kutathmini maendeleo yaliyopatikana katika kudhibiti na kutokomeza kabisa malaria, pamoja na kuhamasisha upya juhudi kuelekea lengo la kutokuwepo tena kifo hata moja kutokana na malaria ifikapo 2015.
Kundi la madaktari wasio na mipaka linasema Malaria ni muuaji mkubwa wa watoto chini ya umri wa miaka mitano katika nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara.
Kundi hilo la wataalamu wa afya linasema
nchi zilizoendelea zinatakiwa kuwa na nia thabiti ya dhati kuzisaidia
nchi zinazoendelea katika kupambana dhidi ya Malaria.
0 comments:
Post a Comment