BABA Mtakatifu Francis, amekubali ombi la Askofu
Mkuu wa Jimbo Kuu la Songea, Norbert Mtega (68),pichani, kustaafu katika utume
wa kuongoza jimbo hilo.
Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari na Katibu
Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Anthony Makunde,
kutoka kwa Balozi wa Papa nchini, Askofu Mkuu Frascisco Padilla, ilieleza kuwa,
Papa amekubali ombi hilo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ombi la Askofu Mtega kwa
Papa, lilitokana na kuwa na matatizo ya kiafya, hivyo kushindwa kuwahudumia
waumini inavyopaswa. Hata hivyo, kikanisa ni siri ya m
tu mwenye hadhi ya
Askofu, anapoomba kwa Papa kustaafu.
“Baba Mtakatifu Francis amekubali ombi la Mhashamu
Askofu Mkuu Norbert Mtega, kustaafu kutoka majukumu ya utawala wa kichungaji wa
Jimbo Kuu la Songea, kwa sababu ya kiafya,” ilieleza taarifa hiyo.
Hata hivyo haikufafanuliwa maradhi yanayomsumbua
Askofu Mtega, ambaye pia kiumri ni miongoni mwa maaskofu wakongwe katika kanisa
hilo nchini.
Katika hatua nyingine, Papa amemteua Askofu
Tarcisius Ngalalekumtwa, wa Iringa, kuwa msimamizi wa kitume wakati kiti cha
Askofu wa Jimbo Kuu la Songea, kikiwa wazi, kwa mamlaka ya kiti
kitakatifu (Mamlaka ya Vatican).
Kwa kawaida, hakuna muda maalum
wa uteuzi wa Askofu Mkuu mwingine kuongoza jimbo, panapotokea askofu amestaafu
utume, lakini huchukua hata miezi sita hadi mwaka kufanyika uteuzi. Hivi sasa
jimbo hilo linaongozwa moja kwa moja kutoka Vatican kwa usimamizi wa Askofu
Ngalalekumtwa.
Askofu Mkuu Mtega alizaliwa katika kijiji cha
Kinyika (Lupanga-Njombe), Agosti 17, 1945. Alipata daraja la Upadri Novemba 14,
1973, aliteuliwa kuwa Askofu wa Jimbo la Iringa Oktoba 28, 1985.
Aliwekwa wakfu na Papa John Paul II Januari 6,
1986, huko Roma II, na miezi miwilli baadae, Machi 9, 1986 alisimikwa Iringa.
Aliteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Songea Julai 6, 1992 na kusimikwa huko Songea
Septemba 20 mwaka huo huo.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment