M To The P akiwa na Mangwea. |
BAADA ya kuwa katika hali mbaya, hatimaye M To
The P amezinduka na kuanza kuuliza maswali juu ya rafiki yake Albert Mangwea, M To The P ambaye alikuwa katika hali mbaya ya kiafya baada ya kudaiwa kutumia vinywaji na madawa ya kulevya kupita kiasi baada ya kuzinduka alimehamishiwa katika wodi ya wagonjwa wa
kawaida leo mchana kutoka ile ya wagonjwa wasiojitambua.
“Kweli anaendelea vizuri sana, sasa amepelekwa
kwenye wodi ya wagonjwa wa kawaida,” alisema Ruta Bushoke, msanii wa muziki wa
kizazi kipya anayeishi nchini humo.
Lakini baadaye Mtanzania mwingine anayeishi
nchini humo alisema M To The P amezinduka.
“Jamaa anauliza Ngwea yuko wapi, sasa
tunashindwa hata kumjibu.
Lakini kuna wengine wamemuambia kwamba atakuja hivi
karibuni, ametoka kidogo,” alisema.
Mangwea na M To The P walikutwa na mkasa ambao
ulipelekea Ngwea kuaga dunia na yeye kubaki akiwa katika hali mbaya.
0 comments:
Post a Comment