Picha ya raia wa jamhuri ya watu wa China na raia wa Tanzania iliyopigwa hivi karibuni mkoani Mtwara.
VURUGU zilizotokea mkoani Mtwara hivi karibuni inasemekana kuwa baadhi ya wachina wanaofanya biashara ndogongo pamoja na wale wanaofanya kazi kwenye makampuni ya kuchimba gesi
wameanza kuondoka katika mji huo.
Habari zilizotufikia hivi punde katika www.jumamtanda.blogspot.com zilieza kuwa baadhi ya ofizi, maduka za raia hao wa jamhuri ya China zinasemekana zimeharibiwa katika vurugu hizo na hakuna
hata mmoja anayeonekana katika maeneo ya ofisi hizo.
"Hatujui wamekimbilia wapi kwa maana hata kwenye
makazi yao hawapo ila wengine walionekana wamejazana kwenye gari aina ya Landcruiser wakielekea njia ya kurudi jijini Dar es Salaam". Kilisema chanzo chetu.
Aidha mtandao huu bado unaendelea na uchunguzi wa kujua ukweli wa hali hiyo ambapo hivi sasa serikali ilifanikiwa kutulinza vuguru hizo kwa mafanikio na kuleta hali ya amani ambayo ilitoweka Mei hivi karibu kuhusu wananchi wa Mtwara kupingaa hatua ya serikali kusafirisha gesi kwenda jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment