NGWEA.BUSHOKE.
Pretoria,Afrika Kusini.
WAKATI taarifa ya kifo cha msanii wa Hip Hop nchini Tanzania Albert Mangwea ikiendelea kugubikwa na utata mwingi, baada ya taarifa za kifo chake kupingana kufua
tia watoa taarifa hizo kutokuwa na vyanzo vya uhakika,Habarimpya.com imeendelea kupata taarifa za kina juu ya kifo cha msanii huyo.
Akizungumza na Habarimpya.com kwa njia ya simu akiwa Pretoria nchini Afrika kusini msanii wa muziki wa kizazi kipya anayeishi nchini Afrika Kusini Bushoke amesema kwamba amesikia taarifa za kifo cha Mangwea lakini hajaamini ingawa hapatikani kwenye simu yake.
Nilikuwa na mipango ya kukutana na Mangwea leo lakini nilipoa amka asubuhi nilijaribu kumtafuta kwenye simu yake sikumpata na kila nilipojaribu tena bado sikupata majibu yoyote, sikuwa na wasiwasi sana kwani nilidhani pengine simu haina chaji na angenitafuta baadaye"alisema Bushoke na kuongeza.
"Niliendelea kumtafuta kwa zaidi ya saa nne ndipo nilipoanza kuwa na wasiwasi, kwani alikuwa na mipango ya kurudi Tanzania na kuna mambo mengi tulizungumza naye nikalazimika kumtafuta rafiki yake wakaribu lakini taarifa aliyonipa ilinishtua sana, jamaa aliniambia kwamba mangwea amezimika".
Bushoke ambaye alikuwa rafiki wa karibu na msanii huyo alizungumzia taarifa hizo kwa uchungu huku akiwa na kwi,kwi kila wakati alisema kwamba, anajiandaa kwenda Hospitali ya St. Hellen ya jijini Johanesburg ili akashuhudie kwa macho yake kama kweli Ngwea amefariki Dunia.
Taarifa za kifo cha msanii huyo zimesambaa katika vyombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania huku picha zake zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii, pamoja na nyimbo zake kupigwa kwenye vituo mbalimbali vya Redio.
0 comments:
Post a Comment