CCM.CHADEMA.
WADAI AMEMUONGEZEA UMAARUFU LEMA NA CHADEMA.
VIGOGO wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwemo wabunge, wamemjia juu Mkuu wa Mkoa (RC) wa Arusha, Magessa Mulongo kwa jinsi alivyoshughulikia kesi ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA).
VIGOGO wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwemo wabunge, wamemjia juu Mkuu wa Mkoa (RC) wa Arusha, Magessa Mulongo kwa jinsi alivyoshughulikia kesi ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA).
Wabunge hao waliliambia
gazeti hili mjini Dodoma kuwa kesi ya uchochezi iliyofunguliwa na serikali
dhidi ya Lema kwa shinikizo la mkuu huyo, itaiathiri kwa kiasi kikubwa CCM.
Mbunge wa Mwibara, Kangi
Lugola alisema kuwa amefuatilia kwa makini chanzo cha kesi ya Lema na hatimaye
kukamatwa na polisi mithili ya gaidi, na kubaini kuwa hulka.
“Mimi
sitaki kuingilia kesi, lakini ukiangalia kuanzia ile inayoitwa video ya vurugu
za Chuo cha Uhas
ibu Arusha na jinsi Mkuu wa Mkoa alivyofika eneo la tukio na
kuondoka, utabaini udhaifu mkubwa wa kiongozi huyo ambao leo unamfanya Lema
aonekane shujaa.
“Leo
tunaingia kwenye uchaguzi mdogo wa madiwani pale Arusha, tunaweza tukashinda,
lakini tutafanya kazi ya ziada kwa sababu tu ya udhaifu wa Mkuu wa Mkoa wa
Arusha,” alisema Lugola.
Mbunge mwingine ambaye
aliomba jina lake lihifadhiwe, alisema alichokifanya Mulongo ni sehemu ya tatizo
kubwa la viongozi wa serikali kujihusisha na ukereketwa wa kisiasa.
“Baba wa Taifa Mwalimu
Nyerere aliwahi kusema kuwa kuna kiongozi, tena hakumtaja jina, kwamba
anapendwa kubebwa, alisema mwacheni abebwe.
Alisema vile kuwazuia polisi
kukabiliana na watu wanaopenda kumbeba kiongozi huyo.
“Mkuu wa Mkoa Arusha na
wengine wanaokabiliana na wapinzani kwa nguvu kubwa bila sababu, hii
inawaongezea umaarufu,” alisema mbunge huyo kutoka moja ya majimbo ya kanda ya
kati.
Mjumbe mmoja wa Kamati Kuu
(CC) ya CCM ambaye pia hakutaka kutaja jina lake, alilaani jinsi mkuu wa mkoa
huyo alivyojikoroga katika kushughulikia mzozo wa Chuo cha Uhasibu Arusha.
“Niliposoma ujumbe wa simu
ya mkononi wa Lema ambao alidai umetoka kwa Mkuu wa Mkoa, nilishangaa sana.
Sijui kwanini amefanya vile,” alisema kigogo huyo.
Aprili 24 mwaka huu, Mulongo
aliliamuru Jeshi la Polisi mkoani Arusha kumkamata Lema kwa madai kuwa
aliwachochea wanafunzi wa chuo hicho cha IAA kumzomea na kumrushia mawe.
Lema alizingirwa nyumbani
kwake na maofisa wa polisi kitengo cha upelelezi na wale wa doria Ijumaa saa
5.30 usiku kisha kuchukuliwa hadi Kituo Kikuu cha Polisi kuhojiwa na kuwekwa
rumande siku tatu hadi Jumatatu wiki hii alipofikishwa mahakamani.
Hata hivyo, madai ya Mulongo
kuwa Lema alichochea wanafuzni hao yanakinzana na ushahidi wa video unaoonesha
kuwa mbunge huyo alitumia kila aina ya ushawishi kuwasihi wasiandamane kufuatia
mwenzao Elly Kago (22) kuuawa na watu wasiojulikana jirani na chuo.
Mapema kabla ya kukamatwa,
Lema aliitisha mkutano na waandishi wa habari akidai kutishiwa na Mulongo
kupitia ujumbe wa maandishi wa simu.
“Umeruka kihunzi cha kwanza,
nitakuonyesha kuwa mimi ni serikali, ulikojificha nitakupata na nitakupa
kesi ninayotaka mimi,’’ ulisomeka ujumbe huo uliotumwa kupitia simu namba 0752
960276 ambayo Lema alidai ni ya Mulungo.
Atisha waandishi
Wakati CCM wakiendelea
kumlalamikia Mulongo kwa hatua zake dhidi ya Lema, kiongozi huyo jana
aliwageukia waandishi wa habari wa Arusha akiwataka wawe makini kipindi hiki,
akidai kuwa nao wanatumika na wanasiasa.
Akihutubia katika sherehe za
Siku ya Wafanyakazi, alisema kuwa ikibainika wanatumika nao watafikishwa katika
vyombo vya sheria.
“Mimi nilikuwa Mkuu wa
Wilaya Bagamoyo, hivi hivi wakawa hawanielewi na ikafika wakati wakanielewa
kwani kuna miongoni mwao tulitaka kuwafikisha katika sheria, lakini tukayaacha
kwa kuwa sisi ndio walezi,” alisema.
Mulongo aliongeza kuwa vitu
ambavyo vinaandikwa si kweli kabisa, na kwamba wataendelea kufuatilia kwani
baadhi ya waandishi wanashirikiana na wanasiasa kuwachafua viongozi wa
serikali.
Alisema baadhi ya waandishi
mkoani Arusha wamekuwa wakifanya kazi zao kwa ushabiki wa kisiasa na kuandika
mambo ambayo hawana uhakika nayo.
“Unapoingia katika mkakati
wa kudhalilisha kiongozi wa serikali unakuwa umeiweka roho yako rehani, kuweni
makini,” alisema.
Aidha alivionya vyama vya
wafanyakazi mkoani Arusha kutoruhusu kutumiwa na watu kwa malengo ya kisiasa na
pia waajiri waache kufanya kazi bila kufuata taratibu na sheria.
TANZANIA DAIM
0 comments:
Post a Comment