BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CHAZ BABA AMVALIISHA PETE YA UCHUMBA MCHUMBA WAKE JUKWAANI.

Charles Gabriel ‘Chaz Baba,’ akimvisha pete mchumba’ke, Rehema Sospeter.

PREZIDAA wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel ‘Chaz Baba,’ juzikati aliendeleza harakati za maandalizi ya ndoa kwa mashabiki wake baada ya kumvisha pete jukwaani mchumba’ke, Rehema Sospeter. 

Tukio hilo lililoshuhudiwa na Amani lilijiri Mei 11, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Business Park, Kijitonyama, Dar, wakati bendi yake ilipokuwa ikitambulisha alba
m mpya, Risasi Kidole.

Akizungumza na paparazi wetu mapema wiki hii, Chaz Baba alisema ameamua kuonesha uamuzi wake huo kuanzia kwa mashabiki wake waliofika ukumbini na kwa wale wasiofika kwa sababu wengi wao walikuwa hawamuamini.
 
“Nilifanya vile kukata vilimilimi ‘coz’ tangu nimegawa kadi za mchango wa harusi, kumekuwa na maswali mengi ambayo yanaashiria wengi hawaamini uamuzi wangu,” alisema Chaz.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: