Habari ndugu zangu
Naombeni
ushauri wenu kuhusu tatizo la dada yangu wa tumbo moja ambalo
sikuwahi kulihisi, kulidhani wala kulijua kwa zaidi ya miaka 20. Kifupi
mimi ni kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 23 ( Natimiza miaka 24
mwezi Juni mwaka huu ). Kwa sasa ninasoma mwaka wa mwisho katika chuo
kikuu kimoja hapa nchini.
Kwetu tumezaliwa watatu dada zangu wawili,
wa kwanza alizaliwa miaka ya sabini ( R.I.P ) na huyu wa pili ambaye
ndie point of discussion, alizaliwa mwanzoni kabisa mwa miaka ya 1980.
Ngoja
niende moja kwa moja kwenye point, siku ya jumamosi iliyopita ( tarehe
27 APRILI 2013 ) saa nne kamili za asubuhi nilienda kumtembelea dada
yangu ( hana mume, mtoto wala sijawahi kusikia chochote kuhusu kuwa na
rafiki wa kiume yaani boyfriend )...
Nilienda
pale kwa ajili ya kupiga mzinga kidogo na nilipanga kurudi hosteli
ambako ninaishi siku iliyokuwa inafuata yani jumapili.
Mida
ya saa sita mchana, aliwasili mdada mmoja ambaye ninamjua kama rafiki
wa karibu wa dada yangu, tulisalimia kisha dada akaja kumpokea mgeni
wake kisha wakaelekea ukumbini, baadaye nikarudi zangu chumbani kwangu
na kuendelea kucheza na laptop yangu.
Yalipita
kama masaa mawili hivi mdada mwingine aliwasili nyumbani na kuingia
moja kwa moja chumbani kwa dadangu .Sikujua kilichokuwa kinaendelea
maana wakati huo nilikuwa chumbani, ila nilikuja kujua baadaye kwamba
kuna mdada mwingine alikuja nyumbani pale .
Nilikuja
kustushwa baadaye na kelele za ugomvi mkubwa sana, zikitoka chumbani
kwa dada yangu ambako nilisikia kelele, na matusi mazito yakiporomoshwa,
vilio na chupa zikivunjwa vunjwa hovyo, sikuwa na jinsi nikaamua
kukimbilia upande kilipo chumba cha dada yangu kutoa msaada.
Kufika
sikuamini kilicho tokea, nilimkuta dada yangu na yule dada mwingine
ambaye nilikuwa namjua kama rafiki yake wakiwa kama walivyo zaliwa,
wamelewa wanagombana na huyu mdada mwingine aliyekuja wakati mimi nimo
ndani, huyu dada mwingine alikuwa anamshambulia yule dada aliyekuja mara
ya kwanza na dada yangu alikuwa anajaribu kumzuia..
Kilicho
nishangaza zaidi kuhusu dada yangu ni kwamba ana u*me ( tena mkubwa tu
kama u*me wa mwanaume rijali, na umevalishwa kinga ), mwanzoni
nilidhani labda amevaa midoli lakini haikuwa hivyo, nii u*me kabisa...
Nilicho kifanya ni kumtoa yule dada aliyekuja mwishoni hadi nje kisha nikarudi zangu chumbani kwangu....
Sikufanikiwa
kuongea na dada yangu usiku huo hadi kesho yake lakini sikuongea
chochote kuhusu kilicho tokea jana yake .Japokuwa aliniomba radhi kwa
kilicho tokea lakini hatukuzungumzia kabisa kuhusu suala la yeye kuwa na
jinsia mbili..
Kusema
ukweli suala hili linanikosesha sana raha na sijui nini cha
kufanya.Nimepanga kutoongea na yoyote wala sitawauliza wazazi wangu
lakini picha hii nitakaa nayo kwa muda mrefu sana, simuoni tena dada
yangu kama nilivyo kuwa naumona hapo zamani..
Naombeni ushauri wenu .
Majidai
0 comments:
Post a Comment