Mkurugenzi
wa upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini DCI Robert Manumba akizungumza
na Wakurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai katika mafunzo ya kufanya
Operesheni za Pamoja kati ya SARPCCO na EAPCCO.Mafunzo hayo yanafanyika
jijini DAR Es Salaam.
Mkurugenzi
wa upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini DCI Robert Manumba akiwa katika picha ya
pamoja na Wakurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai kutoka Nchi mbalimbali za
Afrika ambao wanashiriki mafunzo ya kufanya Operesheni za Pamoja kati ya
SARPCCO na EAPCCO.Mafunzo
hayo yanafanyika jijini DAR Es Salaam.
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi.
Wakurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya jinai kutoka nchi 25 barani
Afrika wametakiwa kutumia vizuri mafunzo ya Operesheni za pamoja ili kuweza
kukabiliana na uhalifu ikiwemo vitendo vya ugaidi na uhamiaji haramu
vinavyojitokeza katika nchi za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika kwa kasi
hivi sasa.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya
Jinai Nchini DCI Robert Manumba wakati akizungumza na waandishi wa habari baada
ya kufungua Mafunzo kwa Wakurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai kutoka
Umoja wa Wakuu wa Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO) Pamoja na Umoja wa Wakuu
wa Polisi Afr
ika Mashariki (EAPCCO) kuhusu kufanya operesheni za pamoja
kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka.
DCI Manumba amesema uhalifu unaofanyika hapa nchini na ukanda huu
wa Afrika Mashariki ndio huo huo unaotokea katika nchi nyingine hivyo
ushirikiano na kubadilishana taarifa kutasaidia kutambua na kuweka mikakati
thabiti ya kuweza kudumisha amani na usalama katika bara la Afrika.
“Kwa mfano suala la Wahamiaji haramu hatuwezi kupambana nalo sisi
wenyewe kwa kuwa wanatoka katika nchi nyingine na hapa wanapita tu kwenda
katika nchini nyingine hivyo lazima tubadilishane taarifa na kuwa na mkakati wa
pamoja wa kuwabaini wanaofanya vitendo hivyo” Alisema Manumba.
Kwa upande wake Mkuu wa Polisi wa Kimataifa INTEPOL kanda ya Afrika
Mashariki kutoka Nchini Kenya Bw.Rego Francis amesema Majeshi ya Polisi yana
wajibu wa kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi ili waweze kutoa taarifa za
uhalifu mapema kwa vyombo vya usalama ili ziweze kufanyiwa kazi mapema kabla ya
matukio kutokea.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Polisi wa Kimataifa (INTEPOL) Tanzania
Kamishna Msaidizi wa Polisi Gustavus Babile amesema Mafunzo hayo ya siku mbili
lengo lake ni kubadilishana uzoefu na kupeana mbinu na kuweka mikakati ya
kufanya operesheni zitakazoweza kuutokemeza uhalifu.
Babile alisema kupitia mafunzo hayo wataweza kuandaa Operesheni
zenye mafanikio zitakazoweza kushirikisha nchi nyingi katika kukabiliana na
Ugaidi, Madawa ya kulevya, wahamiaji haramu, wizi wa magari na uhalifu wa aina
nyingine unaotokea hapa Afrika.
Mafunzo hayo yanafanyika baada ya kumalizika kwa Mkutano wa kumi na nane
wa Wakuu wa Polisi kusini mwa Afrika SARPCCO ambapo katika maazimio
yaliyofikiwa ni pamoja na kufanya operesheni za pamoja baina ya SARPCCO na
EAPCCO.

0 comments:
Post a Comment