DODOMA.
Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli
hivi punde amesema kwamba atabomoa nyumba za wanachama wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) na Chadema bila kujali nyumba ni za kina nani na
amempongeza Rais Jakaya Kik
wete kwa kufanya safari nyingi za nje kwa
kuwa anatafuta fedha za ujenzi wa barabara.
Amesema wamekuwa wakipata wakati mgumu wakati wa kutengeneza
barabara. " Kuna mti mkandarasi alijaribu kuung'a kwa magreda kuanzia
asubuhi mpaka jioni, lakini tulishindwa mpaka tulipowaomba wazee lile
eneo, walipokubali, mti ulianguka wenyewe. Kazi ni ngumu sana, msione
hivi,"amesema Dk Magufuli.
Dk Magufuli amesema kwamba hatajali wala kuogopa kuvunja
nyumba ya mtu yeyote kwa kuwa serikali inafanya hivyo kwa maslahi ya
wanachi wote na taifa kwa ujumla.
Mbali na hayo amewashangaa wabunge wa upinzani kwa kutosifia
juhudi za ujenzi zinazofanywa na serikali ya CCM. "Katika Jimbo la
Mheshimiwa John Mnyika kuna barabara imetengenezwa, lakini sijasikia
akiisifia..., wapinzani wanakosoa kila kitu.
Lazima mkubali ujenzi wa
barabara unapangwa na kusimamiwa na serikali ya CCM, hapo hakuna
ubishi," amesema.
Pia amesisitiza kwamba watu wote waliojenga ndani ya hifadhi
ya barabara umbali wa mita 22.5 na marekebisho ya sheria ya mwaka 2005
ambayo anayehenga ndani
ya hifadhi ya barabara umbali wa mita 30 pia wote watabomolewa kwa kuwa ni kinyume cha sheria.
Wakati akimalizia kuwasilisha hoja yake, Dk Magufuli amesema
kwamba wabunge wote wa upinzani na chama tawala wamechangia vizuri
mjadala wa wizara yake.
Dk Magufuli amesema hayo wakati akihitimisha Bajeti Wizara ya Ujenzi. Chanzo http://www.habarimasai.com
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment