Katibu Mkuu wa Chadema,Dk Wilbrod Slaa
WAKATI Serikali ikiendelea kuwatupia wanasiasa lawama kuhusiana na vurugu za wakazi wa Mtwara wanaopinga hatua ya Rais Kikwete na Serikali kusafirisha Gesi hadi jijini Dar es Salaam kwa njia ya mabomba, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk Willbroad Slaa, amesema kwamba machafuko yanayotokea katika mkoa huo hayasababishwi na mambo ya kisiasa isipokuwa ni umask
ini unaoikabili nchi.
Dk Slaa alisema kwamba umaskini huo unaosababisha vurugu za Mtwara zimesababishwa na CCM tangu zama za kale na si kwa siasa za sasa.
“Yanayotokea Mtwara ni matokeo ya umaskini ambao CCM imewaletea wananchi. Mtwara wanakumbuka ya Mwadui, Geita na North Mara. Wanayakataa”alisema Dk Slaa katika Ukurasa wake wa Tweeter.
Alisema kwamba Wananchi hao wameamua kufanya yote hayo kwa kuangalia wenzao wa mikoa mingine iliyojaliwa kuwa na mali nyingi katika mikoa yao na bado haiwanufaishi matokeo yake inakuwa ni mali yakuwanufaisha wengine bila wao kupata faida yoyote ile.
Katika hatua nyingine Dk Slaa alisema kwamba Serikali isikimbilie kulaumu wanasiasa bali itambue kwamba,siasa chafu zinafanya kazi kama watu ni masikini, lakini kama nchi itakuwa tajiri siasa chafu haziwezi kuwepo. CHANZO http://www.habarimpya.com
0 comments:
Post a Comment