Waombolezaji
katika msiba nchini Zimbabwe walipigwa na butwaa pale mtu aliyekufa
alipoamka wakati wakipita kando ya jeneza lake kutoa heshima za mwisho,
shirika la habari za nchi hiyo limeripoti jana.
BRIGHTON Dama
Zanthe, mwenye miaka 34, aliingizwa ndani ya jeneza Jumatatu iliyopita baada ya
kuwa amefariki nyumbani kwake baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Familia
iliyojawa na huzuni ya mfanyakazi huyo wa usafirishaji ilifunika mwili wake kwa
mablanketi na kufanya mipango ya kumhamishia kwenye mochari ya mjini humo, kwa
mujibu wa ripoti iliyochapishwa katika gazeti la The Herald.
Lakini siku iliyofuata marafiki wa Zanthe na jamaa
zake walisambaratika wakiwa hawaamini pale alipoanza kutembea wakati wakipita
mbele ya jeneza kuaga mwili wa 'marehemu' huyo.
Bosi wa 'marehemu' huyo, Lot Ga
ka alieleza kuhusu
mkasa huo alipobaini mfanyakazi wake alikuwa bado angali hai.
Alisema: "Kwanza niligundua miguu ya Zanthe
ikisogea wakati nilipokuwa kwenye ya foleni kutazama mwili wake. Hili
lilinishitua mno. Kwanza sikuweza kuamini macho yangu lakini baadaye nilibaini
kwamba kulikuwa na kusogea kwa viungo kadhaa katika mwili wake huku
waombolezaji wengine wakiwa hawaamini kinachoendelea."
Gaka, ambaye anaendesha kampuni ya mabasi katika mji
wa Gweru, alisema Zanthe alikuwa hana afya njema kabla ya 'kifo' chake wiki
iliyopita.
Alielezea minsi alivyotembelea nyumbani kwa familia
hiyo kutoa msaada pale mke wa mfanyakazi wake alivyompigia simu kumweleza
kwamba Zanthe alikuwa amefariki.
Alisema: "Zanthe alikuwa katika likizo ya ugonjwa
kwa kipindi fulani na kila mmoja kazini alikuwa akifahamu kwamba hali yake
ilikuwa mbaya.
"Tulimtembelea nyumbani kwake.
"Sikushangaa pale nilipopokea simu kutoka kwa mke
wa Zanthe Jumatatu usiku wiki iliyopita akisema kwamba mume wake alikuwa
amefariki."
Aliongeza: "Nilitembelea maduka mawili yanayouza
majeneza mjini humo kwa ajili ya kuulizia gharama kabla ya kuelekea nyumbani
kwa Zanthe hivyo kuweza kuchukua mwili wake na kuuhifadhi katika mochari.
"Mwili wa Zanthe tayari ulishawekwa kwenye jeneza
na watu walikuwa wakijiandaa kwa utaratibu wa kutoa heshima za mwisho hivyo
mwili wake kuweza kupelekwa mochari.
"Ilikuwa katika wakati huo wa utaratibu wa kutoa
heshima ndipo 'akazinduka'."
Shuhuda mwingine alieleza jinsi familia hiyo ilipovuta
mablanketi hayo kutoka kwenye mwili wa Zanthe huku wakiwa wamechanganyikiwa
kujaribu kumnusuru baada ya kubaini alikuwa bado mzima.
Alisema: "Gaka baadaye aliondoa baadhi ya
mablanketi kutoka kwenye mwili wa Zanthe baada ya kubaini akijitikisa na hii
ilikuwa pale wote tulipobaini kwamba bado kulikuwa na uhai.
"Kisha tuliita gari la wagonjwa ambalo lilikuja
katika muda wa ndani ya dakika saba.
"Hakika ni muujiza na wengi wa watu
hawaamini."
The Herald, ambalo linamilikiwa na serikali ya
Zimbabwe, liliripoti kwamba Zanthe alikaa siku mbili kwenye mashine ya kusaidia
kupumua baada ya kuwa amepelekwa katika Hospitali ya Jimbo la Gweru kufuatia
tukio hilo.
Aliruhusiwa wiki iliyopita na kurejea nyumbani kwake.
Familia ya mtu huyo iliyotikiswa ailieleza ana
kumbukumbu chache tu ya matukio hayo.
Alisema: "Hii ishu inaweza kusimuliwa vizuri na
watu waliofika nyumbani kuhudhuria msiba wangu.
"Sifahamu kilichotokea na ninakumbuka tu kuwapo
hospitalini kwenye mashine za kusaidia kupumua."
Aliongeza: "Kila kitu ni historia kwangu.
"Ninachoweza kuthibitisha ni kwamba watu
walikusanyika nyumbani kwangu kuombolezwa lakini nilipatiwa nafasi nyingine na
niko hai. Najisikia vizuri sasa."


0 comments:
Post a Comment