TANZANIA DAIMA.
MILIO ya risasi, mabomu ya machozi, maji ya kuwasha na silaha za jadi ndivyo vilivyotawala jana katika vurugu zilizotokea mkoani Mtwara na kusababisha mtu mmoja kufariki dunia.
Nyezo hizo ndizo zilizotumika jana katika mapambano baina ya polisi na wananchi waliokuwa wakiandamana huku wakiharibu mali mbalimbali kupinga ujenzi wa bomba la gesi kwenda jijini Dar es Salaam.
Mapambano hayo yalianza katika eneo lililo jirani na Kanisa la Agape mjini Mtwara baada ya wananchi kuanza kuwazomea askari waliokuwa katika doria kutokana na uvumi wa kusimamishwa kwa shughuli zote mjini Mtwara kwa ajili ya kusikiliza hotuba ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, iliyosomwa jana mjini Dodoma.
Mara baada ya hotuba ya Profesa Muhongo, wananchi waliokuwa wakiifuatilia waliamua kuwatumia watoto wanaokadiriwa kuwa na miaka 11 kufunga barabara ya Mkana
lendi iliyopo katika Manispaa ya Mikindani.
Vurugu ziliendelea na kusababisha nyumba ya Mbunge wa Mtwara Mjini Husnein Murji, Ofisi ya CCM Mtwara Vijijini pamoja na nyumba ya mwandishi wa habari wa TBC, Kassim Mikongolo, Ofisi ya Mtendaji Chikongola na Mahakama ya Mwanzo Mitengo kuchomwa moto.
Baada ya matukio hayo wananchi walivamia moja ya nyumba ya wageni iliyodhaniwa kuwahifadhi askari waliotoka nje ya Mkoa wa Mtwara na kutaka kuichoma moto.
Vurugu hizo pia zilisababisha baadhi ya watu kuamua kuharibu madaraja mbalimbali likiwamo lile la Mikindani linalounganisha Mkoa wa Mtwara na Lindi.
Hatua hiyo indaiwa kufanywa kwa lengo la kuzuia watu hasa polisi kutoingia mkoani humo.
Kifo
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Ligula, Mohammed Kodi, amethibitisha kupokea maiti moja na majeruhi ambao hata hivyo hakuweza kutaja idadi yake.
“Ndugu yangu, hivi sasa tupo katika wakati mgumu, siwezi kukuambia ni wangapi wamejeruhiwa ila kifo kilichotokea ni cha mtu mmoja, nitafute baadaye,” alisema.
Huduma za kijamii
Huduma za usafiri, maduka, masoko na hospitali nyingine zilifungwa kuhofia usalama wa watoa huduma kwa jamii au wale waliokuwa wakienda kupata huduma husika.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na Tanzania Daima walisema majira ya saa10 jioni askari walijikusanya katika eneo la Mkana Red na kuanza kuchoma moto vibanda vya wafanyabiashara katika eneo hilo hali iliyosababisha wananchi kuanza kyujikusanya kwa ajili ya kutaka kupambana nao.
Polisi hao wanadaiwa baada ya kumaliza zoezi la kuchoma vibanda vya wafanyabiashara hao walianza zoezi jingine la kuingia nyumba hadi nyumba kwa kuvunja milango na kuwatoa wananchi waliojifungia ndani kuepuka kadhia hiyo na kisha kuondoka nao.
Katika sakata hilo waathirika wakubwa walikuwa kina mama na watoto na waliosalimika walikimbilia katika Msitu wa Naliendele uliopo karibu na kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
“Wanataka kutudhibiti kwa mabomu kwa ajili ya kudai gesi itunufaishe, hii si haki, kwa kweli hatutakubali hali hii, ni bora tufe,” alisema Merina Almas, mkazi wa Mtwara mjini.
Waandishi Mtwara hofu tupu
Hali ya utendaji kazi kwa waandishi wa habari mkoani Mtwara ilikuwa ya wasiwasi kuanzia jana asubuhi, baada ya nyumba ya mwandishi wa habari wa TBC, Kassim Mikongolo, kuchomwa moto kwa madai kuwa mke wake ni askari anayesaidia kuwalinda watu wanaotaka kutoa gesi mkoani humo.
Makao Makuu ya Polisi waongeza nguvu Mtwara
Kutokana na hali kuwa mbaya mjini Mtwara, Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema, alilazimika kutuma timu ya maofisa wa jeshi hilo kutoka makao makuu kwenda kuongeza nguvu.
Kiongozi wa timu hiyo ya kuongeza nguvu mkoani Mtwara, Isaya Mngulu, aliliambia Tanzania Daima kuwa wanakwenda Mtwara kwa kuwa ni jukumu la Jeshi la Polisi kuwalinda raia na mali zao.
Naye Mkurugenzi wa Haki za Binadamu wa Chama cha Wananchi (CUF), Hamis Ismail, alisema waliitegemea hali hiyo, kwa sababu serikali ilishindwa kuchukua hatua ya kuzuia.
“Hali si shwari, kwani hasira iliyochukuliwa na dola pamoja na raia si sahihi, walitakiwa wasubiri michango ya wabunge wengine,” alisema Ismail.
Shule, vyuo vyasitisha masomo
Mkuu wa Shule ya Msingi Shangani, Joseph Kandeo, alisema wameamua kuwarudisha wanafunzi nyumbani kutokana na hali kutokuwa shwari.
“Hali ni tete, hivyo nimeamua kuwarudisha wanafunzi nyumbani kutokana na hali iliyopo, nimewaambia kama hali itakuwa nzuri wafike shuleni siku ya Ijumaa na kama hali ikiendelea hivi wafike shuleni siku ya Jumatatu,” alisema Kandeo.
Chuo Kikuu Kishiriki cha Stella Maris (Stemmuco) pia waliamua kusitisha masomo kutokana na hali kuendelea kuwa mbaya.
Mkuu wa chuo hicho, Dk. Longino Kamuhabwa, alisema asubuhi hali ilikuwa nzuri na wananchuo walisoma kama kawaida lakini baadaye hali ilibadilika.
Wananchi wa Mtaa wa Sinani wamelalamikia polisi kumwaga kitu kinachodhaniwa kuwa ni unga wa sumu unaowasha katika maeneo ya makazi ya watu.
KAMBI YA UPINZANI YACHARUKA, WAZIRI ALAZIMISHA.
MMOJA AFARIKI DUNIA, NYUMBA YA MBUNGE YACHOMWA MOTO.

0 comments:
Post a Comment