Mbunge
wa Arusha mjini Godbless Lema akiwa na mbunge wa Arumeru Joshua Nassari
wametoa damu kwa ajili ya majeruhi walioumia katika tukio la kulipukiwa
na bomu katika Kanisa Katoliki Olasiti Arusha.
Lema amewahimiza wakazi wa
Arusha na vijana kujitolea kwa wingi kuchangia damu ili kuokoa
majeruhi.
Mpaka sasa watu wanaendelea kujitolea kuchangia damu kama
ishara ya kumuunga mkono mbunge wao.
Watu wengi na hasa vijana wamempongeza Lema kwa jinsi anavyohamasisha wananchi kwa lengo la kuokoa majeruhi
0 comments:
Post a Comment