JENERALI mmoja wa jeshi anamshutumu rais Yoweri Museveni wa Uganda
kwa kujaribu kuhakikisha mwanae anarithi madaraka kama kiongozi wa nchi
hiyo, akiwa ni kiongozi wa kwanza wa juu kuelezea wasi wasi wake juu ya
mpango wa mrithi wa madaraka wa rais Museveni baada kuwepo madarakani
kwa karibu miongo mitatu.
JENERALI DAVID SEJUSA.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AP , David Sejusa mmoja wa majenerali
6 wa Uganda alisema katika barua yake ya hivi karibuni kwa mkuu wa
usalama wa taifa kwamba anataka uchunguzi ufanyike juu ya shutuma
kwamba wale watakaompinga mtoto wa museveni kuwa kiongozi ajaye wanaweza
kulengwa kuuwawa.
Jenerali Nyaronda Nyaikirima kamanda wa juu wa jeshi alisema Jumanne kwamba jeshi limedahalilishwa na barua ya Sejusa.
Shutuma hizo na afisa wa juu wa jeshi zimewashtua wengi huko Uganda.
Jenerali Nyaronda Nyaikirima kamanda wa juu wa jeshi alisema Jumanne kwamba jeshi limedahalilishwa na barua ya Sejusa.
Shutuma hizo na afisa wa juu wa jeshi zimewashtua wengi huko Uganda.
0 comments:
Post a Comment