Mei 21,1996 katika ziwa
Victoria,Mwanza Tanzania meli ya Mv Bukoba ilipata ajali na zaidi ya
watu 800 kupoteza maisha yao.
Meli ilizama kilomita 30 kukaribia kutua
nanga kwenye bandari ya mwanza ikitokea Bukoba.
Meli ikuwa na uwezo wa kubeba idadi ya watu 430.
Kwenye first and second
class orodha ya abiria ilikuwa 443 na kwenye third class hakukuwepo
rekodi yoyote .
Takribani 1000 walifariki kwenye ajali hiyo.
WADAU
TUUNGANE KATIKA KUWAOMBEA WENZETU KUANZIA HIVI SASA IKIWA NDIO MUDA
MELI ILIANZA SAFARI KUTOKA BUKOBA MJINI KUELEKEA KEMONDO BAY AMBAPO
ILIENDELEA NA SAFARI KUELEKEA MWANZA AMBAPO ILIZAMA MUDA MCHACHE KABLA
YA KUTIA NANGA JIJINI MWANZA.
JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM inaungana na watanzaania pamoja na kutoa pole kwa wahanga na ndugu, jamaa waliowapoteza wapendwa wao na mwenyezi Mungu awapumzishe mahala pema peponi wote waliotangulia mbele ya haki katika ajali hiyo kwa taifa la Tanzania.
Amina !.
0 comments:
Post a Comment