BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAKETE YAONGOZA KWA KULIMA BANGI MKOANI NJOMBE

JESHI la Polisi Mkoani Njombe Linawashikilia watu wawili kwa matukio mawili tofauti likiwemo la Mmoja kusababisha kifo cha Mwendesha Baiskeli na Mwingine kukutwa na Madawa ya Kulev
ya aina ya Bangi na Kokein.

Kamanda wa Polisi Mkoani Njombe ACP Fulgency Ngonyani amesema tukio la Kwanza limetokea May 28 mwaka Huu Mkazi Mmoja wa Mtaa wa Matalawe anayejulikana kwa Jina la Khalid Chuma [30]amekamatwa akiwa na Madawa ya Kulevya aina ya Bangi yenye Uzito wa Gramu tano na Madawa yanayodaiwa kuwa ni Kokain gramu tatu.

Kamanda Ngonyani amesema tukio la Mtuhumiwa huyo ambaye ni Dereva na Mkazi wa Dar es salaam anaendelea kuhojiwa ili kubaini kiini cha Upatikanaji wa Madawa hayo.

Katika hali ya matukio ya Madawa ya Kulevya Mkoani Njombe Kata ya Matamba Wilayani Makete imeonekana kuongeza katika Kilimo cha Bangi kufuatia kuwepo kwa Idadi kubwa ya Mashamba yaliyobainika kulima zao hilo hatari kati ya Wilaya zote za Mkoa wa Huu.

Aidha Kamanda Ngonyani amesema Tukio la Pili ni la Unyang'anyi wa Kutumia Nguvu ambapo Mtu Mmoja Bwana Benjamin Ndali [33]mkazi wa Malombwe  akiwa anaendesha Pikipiki yake alitishiwa na watu Watano na Kunyang'anywa Pikipiki hiyo.

Kamanda Ngonyani amesema kuwa Tukio hilo limetokea may 28 mwaka Huu katika Kijiji cha Lyamkena Makambako baada ya Mtu huyo kukutana na watu watano waliokuwa na zama mbalimbali yakiwemo Mapanga kisha kumtishia na Kumpora Pikipiki yake yenye Namba za Usajili T.474 BFM Aina ya Star LG.

Amesema hakuna aliyekamatwa hadi sasa kuhusiana na Tukio hilo hivyo jeshi la Polisi Linaendelea na Upelelezi Juu ya watu waliohusika na Uporaji wa Pikipiki hiyo.

Tukio la Tatu Kamanda Ngonyani amesema Mtu Mmoja mpanda baiskeli Ephron Sanga amefariki dunia baada ya Kugongwa na Basi aina ya Scania mali ya Kampuni ya Nganga inayofanya safari zake kutoka Mbye-Dar.

Kamanda Ngonyani amesema Tukio hilo limetokea leo Mei 29 mwaka Huu majira ya Saa Mbili Asubuhi katika Eneo la Mjimwema Makambako karibu na Stendi Kuu ya Mabasi mjini humo

Jeshi la Polisi limeshilkilia Dereva wa Gari hilo anayejulikana kwa Jina la Andrew Salo mwenye umri wa Miaka 33 mkazi wa Mbeya kwa kusababisha Kifo cha Mfanyabiashara Huyo kwa Kuendesha gari kwa Uzembe katikati ya Mji wa Makambako

Na Gabriel Kilamlya
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: