Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na
Maendeleo (WAMA) na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkaribisha kwa
mazungumzo Daktari bingwa wa watoto Jerome Paulson, Mkurugenzi wa Afya
ya watoto na Mazingira kutoka Chidren's National Medical Center ya huko
Washington nchini Marekani aliyemtembelea Mama Salma kwenye ofisi ya
WAMA jijini Dar es Salaam tarehe 21.5.2013. Dr. Jerome amekuja Tanzania
kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa Madaktari Bingwa wa watoto hapa nchini
kuhusu afya ya mtoto na mazingira kufuatia makubaliano aliyoyafanya na
Mama Salma wakati alipotembelea taasisi hiyo huko Washington mwaka 2012.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Daktari Bingwa wa watoto Jerome
Paulson aliyeambatana na Mkewe pamoja na viongozi wa Chama cha Madaktari
wa watoto hapa Tanzania (Paediatrc Association of Tanzania-PAT). Kutoka
kushoto ni Dr. Augustino Masawe akifuatiwa na Rais wa Chama cha
Madaktari wa watoto nchini (PAT) Dr. Rodrick Kisenge, Mrs Jerome na kwa
nyuma ni Dr. Francis Furia,Mjumbe na Dr. Hadija Mwamtemi, Mwekahazina wa
chama hicho.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Daktari Bingwa wa
Watoto Jerome Paulson kutoka Marekani na Viongozi wa Chama cha Madaktari
wa Watoto hapa Tanzania kwenye ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya
Wanawake na Maendeleo, WAMA, tarehe 21.5.2013.
0 comments:
Post a Comment