MTANZANIA.Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akijibu hoja za wabunge
waliochangia makadirio ya matumizi ya Wizara yake kwa mwaka 201
3/14,
bungeni Dodoma, jana. Picha na Emmanuel Herman
SERIKALI imetangaza kuwa sekta binafsi 12 nchini, zimekubali kuongeza
kima cha chini cha mshahara kwa wafanyakazi wake. Taarifa hiyo ilitolewa
bungeni jana na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka wakati
akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa
fedha 2013/14.
Kabaka alizitaja sekta hizo kuwa ni ujenzi, shule
binafsi, nishati, viwanda na biashara, hoteli na huduma za majumbani.
Nyingine ni ulinzi binafsi, madini, afya, uvuvi, usafirishaji,
mawasiliano na kilimo.
Katika hotuba hiyo Kabaka alisema,
mishahara katika sekta ya viwanda na biashara inaongezeka kwa asilimia
43.8, wakati hoteli na huduma za majumbani imeongezeka kwa asilimia
55.2.
Kabaka alisema mishahara katika sekta ya ulinzi binafsi imeongezeka kwa
asilimia 46, madini asilimia 25.2, uvuvi na huduma za majini asilimia
21.2, usafirishaji inaongezeka kwa asilimia 49 na sekta ya kilimo
asilimia 42.0.
Kabaka alisema sekta nne mpya zilizoanzishwa
ambazo ni ujenzi, shule binafsi, nishati na mawasiliano nazo kima cha
chini kimeongezwa.
“Viwango hivyo vipya vya kima cha chini cha
mshahara, vitaanza kutumika Julai mwaka huu na vitatangazwa rasmi katika
gazeti la Serikali,” alisema Kabaka.
Kwa mujibu wa Waziri Kabaka, nyongeza hizo za mishahara zimezingatia tija na hali ya uzalishaji na utoaji wa huduma nchini.
Alisema
viwango hivyo pia vimezingatia uwezo wa waajiri na wazalishaji katika
kila sekta, mfumuko wa bei na kulinda ajira nchini ili wafanyakazi
wasipunguzwe kazi.
Kabaka alisema wizara yake imeendelea
kuimarisha utaratibu wa ukusanyaji wa ajira na kwamba mwaka 2012/13
jumla ya ajira 27, 4030 zimepatikana.
Kabaka alisema kati ya hizo, ajira 8,603 zilitangazwa na sekta binafsi wakati ajira 56,746 zilitolewa na Serikali.
Kuhusu
ajira za wageni, Kabaka alisema wizara imeandaa rasimu ya Muswada wa
Sheria ya Vibali kwa ajira za wageni ambao utawasilishwa bungeni
mwakani.
“Lengo la Muswada huo ni kuwa na sheria moja ya
kusimamia masuala ya vibali vya ajira za wageni na hivyo kuondoa utata
na migogoro katika utaratibu unaotumika sasa,” alisema.
Alisema katika mwaka huu wa fedha, wizara yake ilipokea na kushughulikia maombi ya ajira za kigeni 6,424.
Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, pamoja na mambo mengine imetaka utaratibu wa utoaji ajira kwa wageni uangaliwe upya.
Kamati hiyo ilisema kwa sasa ajira hizo zimekuwa zikitolewa kiholela hasa katika kazi ambazo Watanzania wanaweza kuzifanya.
Maoni
ya kamati hiyo yalitolewa na mwenyekiti wake Jenister Mhagama, ambaye
pia ni Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Peramiho.
“Kamati inasisitiza Serikali kuharakisha sheria ya kusimamia ajira za wageni wanaokuja kufanya kazi nchini.
“Kamati
pia inaitaka Serikali kusimamia kikamilifu haki za wafanyakazi katika
sekta binafsi, ikiwemo mifumo ya ajira na mafao yao.
Wizara ya Kazi na Ajira imeomba kuidhinishiwa Sh. bilioni 14.958 kwa ajili ya maendeleo na matumizi ya kawaida.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment