SIKU chache baada ya msanii wa filamu Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ kunaswa kwenye mtego wa kujiuza, sasa ameamua kubadilisha mfumo wa maisha aliyokuwa akiishi zamani na kuwa na mwingine mpya.
Akiongea na mwandishi wa habari
hii, Aunty Lulu alifunguka kuwa kwa sasa ameamua kubadilika kwani kama
ni starehe amefanya sana pamoja na uchafu mwingi ila kutokana na mtego
wa kujiuza kumnasa na ushauri aliopewa na familia yake, amebadilika na
sasa amegeukia kwenye ujasiriamali.
“Yaani kutokana na mtego wa kujiuza
nimeamua kubadilika kwa sababu jamii ilinichukulia tofauti sana hivyo
nikaamua kufanyia kazi ushauri wa familia yangu niliokuwa nikipewa kila
siku lakini nikawa naukataa.
Kwa sasa nafanya ujasiriamali na ninafurahia maisha haya kuliko yale niliyokuwa nikiishi zamani.
Aunty Lulu kwa sasa anamiliki duka la
vipodozi na ni wakala wa kutoa na kuweka fedha kwa kupitia mitandao ya
simu za mkononi maeneo ya Kinondoni Kanisani, Dar ambapo ndipo anashinda
kwa sasa na kwa mujibu wake ameachana kabisa na kujiachia kwenye
sehemu za starehe na kufanya mambo yasiyotakiwa katika jamii.
CHANZO http://masainyotambofu.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment